Ajali Dar: Chenge adaiwa kujuana na mmoja wa marehemu
Frederick Katulanda,Mwanza
SAKATA la ajali ya gari la Andrew Chenge ambalo limesababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya ndugu wa wasichana hao kudai kuwa Chenge alikuwa akimfahamu mmoja wa marehemu.
Chenge ambaye alikuwa Waziri na Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliingia matatani baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga "bajaji" usiku wa kuamkia juzi na kuua wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na mmiliki wa saluni ya kike na Vicky George Makanya.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza baadhi ya ndugu waliohojiwa na Mwananchi Jumapili akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky.
Akizungumza na Mama wa marehemu Vicky, Nazifa Kambi nyumbani kwao Iloganzala ambako kuna matanga alisema amesikitishwa na taarifa za upotoshaji zilizoeleza kuwa mwanae na rafiki yake walikuwa wakienda Zanzibar kwa ajili ya kufunga ndoa jambo ambalo alilipinga na kueleza kuwa alikuwa akija Mwanza baada ya kutoka Zanzibar ambako walikwenda kununua vifaa vya saluni ya mwenzake.
"Ajali hii inanipa mashaka makubwa kutokana na kupokea taarifa za kupotosha za kufunga ndoa," alisema.
Alisema pia amepata taarifa kutoka kwa wafanyakazi wenzake kuwa Chenge walikuwa wakifahamiana na Vicky na kwamba kila mara alipokuwa akifika Mwanza Hotel alikuwa akimtaka kumhudumia vinywaji yeye.
Nazifa alisema marehemu Vicky ambaye alikuwa mfanyakazi wa Mwanza Hotel katika kitengo cha King Casino ambayo kwa sasa inajulikana kama The Stone, hata yeye mwenyewe aliwahi kumsikia mwanaye kuhusu mbunge huyo kumtaka atoke nyumbani kwenda kumhudumia siku ambayo hakuwa kazini.
Ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo ili kupata nini kilichosababisha ajali hiyo.
Kwa upande wa msemaji wa familia ya Beatrice, kaka wa marehemu, Andrew Costantine akiwa Kiseke kwenye matanga alisema wanachofahamu wao ni kuwa dada yake amepatwa ajali akiwa njiani kurejea hotelini walikofikia ya JVL Hotel iliyopo Mwananyamala wakati wakitoka Oysterbay kwa ajili ya kuchukua mizigo yao tayari kwa kuondoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.
Andrew alieleza kuwa tayari marehemu na rafiki yake walikuwa wamekwisha kutoka Zanzibar ambako walikwenda kununua bidhaa na vifaa vya saluni ya kike ambavyo vimekutwa hotelini walikokuwa wamefikia.
Alisema marehemu hakuwa amekwenda kufunga ndoa Zanzibar kwa vile alikuwa na mume wake ambaye ni mzungu raia wa Marekani na kwamba mpaka anafikwa na mauti mme wake alikuwa nje ya nchi.
Alisema habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa walikuwa wakienda kufunga ndoa siyo za kweli.
"Wakati wakiondoka alimuaga rafiki yake Khadija Hassani ambaye ndiye alimuachia nyumba yake na wakati akiwa Zanzibar alimtumia fedha kwa ajili ya kuwalipia ada ya shule watoto, sasa mambo mengine hakuna anayejua tunaomba uvumulivu msiba uishe," alieleza.
Alisema mpaka sasa Chenge ameahidi kusaidia familia kusafirisha miili ya marehemu hao, lakini bado hawajapokea lolote kutoka kwake na wanaendelea kumsubiria wakati polisi wakikamilisha taratibu za uchunguzi huku na wao wakijipanga kusafirisha miili ya ndugu zao.
Msiba hii imeacha simanzi Jijini Mwanza na kuwa gumzo kubwa huku ukizua minogono ya hapa na pale na baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wengine wakishangazwa na tukio hilo na jinsi jeshi la polisi lilivyounda tume kushughulikia ajali hiyo tofauti na ajali nyingine.
Marehemu hao waliondoka Jijini Mwanza Machi 24, mwaka huu kwa safari ya kibiashara Dar es salaam na baadaye Zanzibar na walikuwa wakitarajiwa kureja Ijumaa Machi 27, Beatrice ameacha watoto wanne ambao wanasoma shule tofauti za bweni na mwenzake Vicky ameacha mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Chege kwa simu jana hazikuzaa matunda jana.
My Take; I wonder if it was a coincidence kuwa Mh Chenge amejikuta akimgonga mtu aliyekuwa akimtafuta kila alipokuwa akienda Mwanza,kama alikuwa akimwita akampe huduma hata wakati akiwa off ama likizo basi nitashangazwa kama hawakuwa na mawasiliano wakati mwanadada huyo akiwa hapo Dar.
Hii ni dalili kwamba kuna mambo mengi yakawa yamefichwa,unaweza kuwa ni set up kama huyo mwanadada alizidi kumwandama Mheshmiwa,mheshimiwa akaona ni kama blackmailing.
Toka mwanzo picha za tukio la ajali na maelezo vinapingana sana,ukichanganya na ukweli kuwa dereva amepotea na merehemu hawawezi kutoa ushahidi,labda hayo mambo ya insurance na mengineyo ni ya ku tutoa nje ya pointi.