Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku zote unatakiwa ukane ,hivyo kama huna habari basi hiyo ndivyo ilivyo,unatakiwa ukatae mashtaka , si unaona wahalifu wote wanakataa makosa yao ,maana katika kukataa wale wanaokushitaki wakizubaa tu umetoka na kurudi uraiani ,sasa hapa katika kesi hii ili kupindishwa pindishwa ushahidi itabidi utolewe kiaina , na kama chenge tayari ameshanunua vifo vya hao waliokufa basi hapo dau lake si dogo kwa kila kichwa,halafu kama dereva hajapatikana inaweza ikaifanya hii kesi kuwekwa kiporo kwani ushahidi utakuwa hautimii mpaka dereva wa Bajia apatikane.polisi wakisema bajaji iligongwa kwa nyuma wakati kule inaonekana gari ya Chenge imeumia ubavuni ,ushahidi wa polisi utakuwa wa uongo,Anadunda yupo mtaani kapata dhamana na kakana mashitaka yote matatu. Upo hapo?
Taarifa kutoka kwenye mazishi ya Beatrice huko Mwanza zinaeleza kuwa kaka wa marehemu aitwaye Cosntantine, amewaeleza waombolezaji kuwa Chenge alikuwa pamoja na marehemu hao maisha Club wakikata kinywaji. Anasema awali, Chenge alimpigia simu dada yake na kumtaka wakutane hapo na dada huyo aliamua kwenda na rafiki yake. kwa mujibu wa maelezo ya Costantine, kulitokea kutoelewana na dada yake na rafiki yake wakaamua kuondoka na kibajaj lakini Chenge aliingia kwenye gari lake na kuanza kuwafukuza.
Kwenye mazishi chenge aliwkilishwa na rafiki yake kipenzi Clementi mabina, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. Mabina aliwasilisha rambirambi ya Sh lakini tano kutoka kwa Chenge na kueleza kuwa Change alipanga kuhudhuria mazishi lakini ameshindwa kutokana na kukabiliwa na kesi.
Akiwasilisha salamu za Chenge mabina alisema anaitaka familia kuwa na subira wakati huu na kuacha kusikiliza tetesi za mitaani kuhusiana na ajali hiyo kwani yeye hakukusudia kuwagonga waliokuwa kwenye bajaj
Kuhani,
Nadhani Kiswahili hakijaweza ku catch up na kiingereza...
Hii "kweli si kweli" ndo plea taking -- yaani " guilty or not guilty"
Bado ungejibu " guilty?" unajua ambacho kingefuatia ni kusomewa facts of the case na baadae sentence ...jela.Sidhani Chenge anataka kwenda jela upesi hivyo!
Hilo hakushitakiwa nalo ,maana inategemea yule anaekwenda kukushitaki au kukufungulia kesi ,pemgine jamaa hakuzibandika ,sasa ,pengine hilo polisi wameona haliwahusu au halihusiani na vifo au ni jepesi na wako wengi ambao wanaendesha bila ya kuwa na bima ,hapo huwa ndipo wanapopatia mlo wa siku,hivyo wakianza kuwakamata kamata watakosa ulaji lazima mambo mengine uwe unatumia akili ili usije baadae ukapoteza uwekezaji. Hapo inaonyesha polisi wa usalama wamewekeza 😀Nimesoma magazeti mengi sana yanayoripoti habari za Chenge na ajali hii yenye utata, sijasoma mahali popote panapoonesha kwamba Chenge amesomewa shitaka la kuendesha gari ambalo bima yake imekwisha muda wake tangu mwaka 2007. Wameonesha makosa ya kugonga na kuua tu. Au kosa hili wameliruka? Au nimesoma vibaya!
Wadau hili nalo limekaaje?
kufuatana na taarifa za magazeti ya leo, inasemekana bima ya 2008 ilonekana ndani ya gari! na ya 2008 -2010 (ya miaka 3) imeonyeshwa kwa polisi ilikatwa NIC. SIJUI SIKU HIZI MTU ANAWEZA KUKATA BIMA YA GARI YA MIAKA MINGAPI NIC. ninavyofahamu bima huwa ni ya mwaka moja moja au chini ya hapo ikitegemea matumizi ya gari.
kwa bingo sio jambo la ajabu kukata bima baada ya kupata ajali.
macinkus
Taarifa kutoka kwenye mazishi ya Beatrice huko Mwanza zinaeleza kuwa kaka wa marehemu aitwaye Cosntantine, amewaeleza waombolezaji kuwa Chenge alikuwa pamoja na marehemu hao maisha Club wakikata kinywaji. Anasema awali, Chenge alimpigia simu dada yake na kumtaka wakutane hapo na dada huyo aliamua kwenda na rafiki yake. kwa mujibu wa maelezo ya Costantine, kulitokea kutoelewana na dada yake na rafiki yake wakaamua kuondoka na kibajaj lakini Chenge aliingia kwenye gari lake na kuanza kuwafukuza.
Kwenye mazishi chenge aliwkilishwa na rafiki yake kipenzi Clementi mabina, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. Mabina aliwasilisha rambirambi ya Sh lakini tano kutoka kwa Chenge na kueleza kuwa Change alipanga kuhudhuria mazishi lakini ameshindwa kutokana na kukabiliwa na kesi.
Akiwasilisha salamu za Chenge mabina alisema anaitaka familia kuwa na subira wakati huu na kuacha kusikiliza tetesi za mitaani kuhusiana na ajali hiyo kwani yeye hakukusudia kuwagonga waliokuwa kwenye bajaj
Fundo Uchuro
Umeishapona? Pole sana!
We u mchuro na mchawi! Ulitaka asipone umle nyama.
Fundo Uchuro
Umeishapona? Pole sana!
Kupona nini? Mbona sina habari kuwa nilikuwa naumwa? Au Uwiano Maalum yuko sahihi?
WomenofSubstanc,
Ni kweli lugha yetu haitoshelezi mahitaji ya mawasiliano ya kitaalam na ndio maana hata sheria zinaandikwa Kiingereza. Lakini hata maneno guilty/not guilty nayo tabu?
Hatuwezi kusoma shitaka kwa Kiswahili sahihi, tutaweza kuandika sheria na hukumu kwa Kiingereza cha watu?
Kuhani, unashtakiwa kwa kosa la kusababisha....kweli, si kweli? KWELI, NASHITAKIWA!
Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Je, unakiri kosa, au hukiri?
Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Ikirari (plea) yako ni nini, una hatia, au huna hatia?
Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali...Je, unakana shitaka, au hukani?
Kigumu nini hapo?