Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Mimi bado ninajiuliza kwa nini hawa mabinti walifariki? Kwa jinsi simu za mkonononi zilivyojaa, kwa nini hakuna aliyetafuta msaada wa hospitali? Bila shaka mtuhumiwa alikuwa na uwezo wa kupigia simu hizo hospitali kama zipo!Kama hazipo, tunafanya nini kuhakikisha kuwa pale panapotokea ajali majeruhi wanapatiwa huduma haraka iwezekanavyo? Hizi idadi za vifo za kutisha kila panapotokea ajali kweli hazitustui? Badala ya kukazania tu kuwakamata wanaosababisha hizo ajali juhudi nazo zifanywe kuhakikisha kuwa maisha ya wenzetu yanaokolewa. Watu wanakufa kwa sababu hakuna anayejua kufunga tourniquet kuzuia damu kupotea? Hao polisi wanapopata taarifa ya ajali, je wanawasiliana na hospitali ili watume watu wa huduma ya kwanza? Kama tunashindwa kabisa basi kwa nini hao mapolisi wa traffic wasiongezewe basic training ya first aid? Hii biashara ya kwamba ajali maana yake kifo ni lazima itafutiwe ufumbuzi.

Amandla..........

...maswali mazuri. Hivi Tanzania ukipiga simu 999 inapokelewa na nani? mbona Zimamoto, na polisi huchukua masaa kuwasili kwenye eneo la tukio (kwa Chenge walitumia 45mins kuwasili)? Ambulance ndio sahau kabisa...!
 
Duh,wakuu mnaongelea mambo ya 999.Nadhani mtakuwa mmefocus mijini tu(hasa Dsm).Huko vijijini hata hizo gari zilizopo ni za kuzisukuma mita za kutosha ili ziwake.Huko habari ya gari la zimamoto cjui dharura hawalijui.Kwa jinsi hali inavyozidi kuwa ngumu huko vijijini ndo maana vijana wanazidi kumiminika mijini kila siku huku wakiwa hawana ajira wala mitaji.Kwa Dar es salaam tutasema mengi sana,ila kikwazo kikubwa ni UHOLELA wa mji.Watu wanajenga tu(hasa uswahilini) utadhan wamepaki magari...Hakuna barabara za kueleweka,ramani miji cjui!!Sasa najiuliza hata kama mtu akapiga hiyo 999 itakuwaje.Kwanza kupatambua hapo alipo anayehitaji huduma ni shughuli.
 
Hii ajali imetokea mjini. Imehusu mtu anayetambulika katika jamii. Sasa kama katika hali hiyo, huduma ya tahadhari hamna basi huko vijijini ndiyo hatari kubwa. Kama mahali ambapo basic infrastructure ipo ( simu, vituo vya zimamoto, ambulance, barabara n.k.) tunashindwa hii inaeleza nini kuhusu priorities zetu?
 
...maswali mazuri. Hivi Tanzania ukipiga simu 999 inapokelewa na nani? mbona Zimamoto, na polisi huchukua masaa kuwasili kwenye eneo la tukio (kwa Chenge walitumia 45mins kuwasili)? Ambulance ndio sahau kabisa...!

999 Duh! Mbu itakuwa uliondoka bongo siku nyingi sana,siku hizi inatumika 112zaidi ya miaka 10.
 
walikuwa wakinywa baa gani au hoteli gani???

Kwa kifupi Vicky ambaye sasa Imebainika kuwa pia alikuwa akijulikana kwa Jina la HALIMA pamoja na mwenzake Beatrece walikuwa pamoja na Mkuu Chenge kule MAISHA CLUB. na huko walienda kwa kuitwa na Chenge kwani taarifa zilizopo sasa ni kuwa walipigiwa simu kwenda huko na walipofika walikuta Vijicent anacheza Darts hapo Maisha Club.
 
"Hizo ndizo habari za awali kuwa walikuwa wanafukuzwa na nadhani katika ile michezo ya kijinga ya kuwatishia na kuwapiga mkwara. Kwa gari linalokwenda kwenye mwendo wa 80KM/h nadhani ni mchezo wa kijinga."
__________________

MKJJ: Pengine haukuwa "mchezo wa kijinga" na ilikuwa ni dhamira ya kumwonyesha huyo dada wa Constantine kwamba Andrea -- bingwa wa radar, Meremeta etc -- siyo mtu wa kukataliwa na "changu doa" kama huyo!

Lakini maelezo ya Mpita Njia yanaleta maswali mapya -- kwamba Andrea hakusema ukweli pale alipotamka kwamba kumfahamu kwake Vicky ni kule Mwanza tu akimhudumia katika Hoteli, na si zaidi ya hapo. Kwa nini alidanganya -- hakusema walikuwa pamoja masaa machache kabla.

Kuna kitu nadhani ujamuelewa 'mpita njia' aliyesema Vicky na Chenge wanafahamihana ni mama yake na Vicky ajulikanaye kwa jina la Nadhifa kambi, andrew ni kaka yake na Beatrece aliyeko Mwanza lakini kaka yake mwingine ambaye aitwaye January Costantine huyu ametoka Dar naye ndiye kaja na hilo la kuthibitisha kuwa walikuwa maisha Club walienda kwa kupigiwa simu na Chenge na walimkuta akicheza Darts na ajali imetokea wakati wakifukuzana.
 
Hatimaye mmiliki wa Bajaj ya ajali ya Chenge amejitokeza na kujisalimisha polisi na polisi bila hiyana wamemtia ndani

Source: Radio One
 
999 Duh! Mbu itakuwa uliondoka bongo siku nyingi sana,siku hizi inatumika 112zaidi ya miaka 10.

Mkuu, kuna maneno ambayo hayabadiliki na wakati. Kwa mfano 999 si namba unayopiga bali ni zaidi ya hapo. Tunaposema gari la 999 ina maana kuwa ni gari la polisi lenye taa juu na king'ora. Hii itabaki hivyo hata kama namba ya emergency imebadilika. Mifano mingine ni:
1. Chupa ya thermos haina maana iliyotengezwa na thermos bali vacuum flask yeyote hata ya kichina.
2. Green vest jeshini si T-shirt ya kijani bali ni T-shirt yeyote ya jeshi ndiyo maana si ajabu kuambiwa uvae Green vest nyeupe!
3. Dala dala ilitokana na nauli ya shilingi tano ( wakati huo tukiita dala) iliyokuwa ikitozwa zilipoanzishwa. Nauli hata ibadilike vipi lakini bado haya magari yataitwa dala dala.
4. Kituo cha basi cha Kwa Remy kitabaki hivyo hata Remy akihama.
n.k. n.k.

Kutokana na hii mifano si ajabu mtu akikwambia kapige 999 wakati anakusudia upige 112!
 
Thanks for the analysis
Kawa kuwa KOVA ameunda tume hapa kuna harufu ya Ufisadi and I don't know anaweka precedence gani kwa JAMII that is a traffic case yenye jinai kwa kuunda tume kuna mushikeli mkubwa hapa. Tutabakia na maswali mengi kuliko majbu. Kamanda Kivuyo was a total mess hakuweza kutuambia kwa nini alikwenda kusimamia kazi ambayo at most RTO in the worst case scenario angeenda kwenye site ya tukio kama yule inspector angechora ramani yenye utata. Kwa akili ya kawaida Vijisenti angepelekwa kwa Pilato na Mahakama ingetoa taswira sahihi vinginevyo its another political comedy. Let us wait and see that is we shall cross the Bridge when we come to it.

Mwanakijiji!
Kama ilivyo hapo juu nilisema kulikuwa na harufu ya ufisadi. Na yametimia!!! Nilisahau kupost kilichotekea lakini leo nimepata nafasi kidogo si unajua tena kuna bonge la Passover as from leo jioni!!

Tume iliyoundwa na KOVA ambayo alitumbukia SACP- Peter Kivuyo(Kama alishapanda cheo zaidi sijui) ilikuwa ni bosheni ya kumsaidia Vijisenti si unajua tena washikaji mtindo wa CCM.
Kesi hii ingepitia kwa DPP ISINGEPELEKWA mahakamani lakini kwa sababu trafic case hazipitii kule kwa Feleshi! Andrew Chenge alikuwa mwanasheria Mkuu kwa hiyo alishajiwekea wigo asishitakiwe na hilo tumelishihudia kwenye rada kwani Hosea{msukuma aliwekwa PCCCB amlinde ANDEREA Chenge , Dr. IDRIS RASHID na wenzake wasiende kwa PILATO)
Kijana Feleshi {DPP)aliye na uhusiano wa karibu na Edward Hosea linked to CHENGE alipekua vipengele vya Sheria na sio bahati mbaya alipopelekwa mahakamani alishtakiwa chini ya sheria Kifungu No. 41 ambacho adhabu anayoweza kupewa ni faini ya TSHS.15,000/= au kifungo cha miaka miwili jela na lazima atapigwa faini akale vijisenti kwa amani hiyo ndiyo sheria!!kwa sababu ni mara ya kwanza na yeye ni Mbunge tena mwenye Vijisenti mpaka Ulaya wanamtambua.

Mallya aliyesadikiwa aliendesha gari na hakuwa amelewa wala hakuna aliyemwona akiendesha hilo gari lilomwua marehemu Wangwe alishitakiwa chini ya kifungu No.40 ambacho adhabu yake ni faini na kifungo cha miaka mitatu na amefungwa ila nasikia amekata rufaa.

Sheria inafuatwa kulingana na wewe ni nani ehee!!! Chenge alilewa Polisi chini ya Kivuyo hawakupima kiwango cha ulevi;pili alikuwa hana leseni;tatu gari haikuwa na Bima wala haijalipiwa Road LICENCE na inatembea barabarani for two years wala hakuswekwa lupango kama Mallya!!!!

Nashawishika kuwaambia walalahoi tuungane na Mh. Pinda mtoto wa MKUBWA au mkubwa mwenyewe au Mbunge au Pedege, akitenda kosa ni sharti auwawe papo hapo kwani ukimpekeleka Poilsi inakula kwako tumeshuhudia kuanzia mtoto wa RUPIA aliua baba yake akiwa Katibu mkuu Ikulu akaachiwa , Marehemu Ditto Captain wa JWTZ akitumia bastola yenye silencer kuua dereva mndengereko akapewa dhamana na Kikwete akabariki hilo!! Mungu akachukia akampeleka mwenyewe mbele ya haki!!! Chenge kaua wadada wawili aliokuwa anapeta nao kule Mwanza kaachiwa!!! Mweee!! siingilii mahakama lakini habari ndio hiyo lazima atapigwa faini na waandishi waendelee na njaa zao si mliskia pale Mhakama ya Kinondoni yule Mamaa si alisema mchana kweupee!!!

Alisema marehemu Nyerere!! Haka kanchi kanauka rushwa that was in 1995 je leo baada ya almost 15years kananukaaaaa! tena kimbaa!!!!
 
Mara nyingi nasikia MAKUNDI YA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU. Naomba nifahamishwe kutokana na ujinga nilionao; makundi haya yanafanya kazi kwa faida ya nani na mipaka yake ya utendaji kazi ikoje. Nauliza hivi kwa sababu naamini kama makundi yanatenda kazi kuhakikisha kila mtu hususani raia wa kawaida na walalahoi ambao ni wengi wanapatiwa haki ama kutetewa pale inapooneka kuwa sheria inapindishwa kwa manufaa ya mtu ama kundi fulani ama kwa lengo la kumkandamiza mwingine. Inakuwaje mtu anaamua kumuua mwenzake whether kwa kukusudia ama pasipo kukusudia lakini sheria inakuwa twisted ili kumlinda mhusika na makundi haya yanakaa kimya bila hata kuonyesha ishara ya kukemea mambo hayo? Sheria ni utaalamu, naamini makundi haya yangejitahidi kutoa maelekezo na kuelimisha japo kidogo kwa wale wanaoonekana kuonewa lakini hawana uwezo ama uelewa wa mambo ya kisheria.
 
Kwani swala la Chenge alikuwa na hawa akina dada maisha klabu kabla ya ajali au usiku ule limeishaje, hakuna watu wa kulitolea ushahidi hilo au walikuwa watatu tu hata wahudumu hawakuwepo??? au ni tetesi hakuna ushahidi kwamba walikuwa maisha kabla ya vijisent kuamua kutoa roho zao.
naomba mwongozo.
 
Mwanakijiji!
Kama ilivyo hapo juu nilisema kulikuwa na harufu ya ufisadi. Na yametimia!!! Nilisahau kupost kilichotekea lakini leo nimepata nafasi kidogo si unajua tena kuna bonge la Passover as from leo jioni!!

Tume iliyoundwa na KOVA ambayo alitumbukia SACP- Peter Kivuyo(Kama alishapanda cheo zaidi sijui) ilikuwa ni bosheni ya kumsaidia Vijisenti si unajua tena washikaji mtindo wa CCM.
Kesi hii ingepitia kwa DPP ISINGEPELEKWA mahakamani lakini kwa sababu trafic case hazipitii kule kwa Feleshi! Andrew Chenge alikuwa mwanasheria Mkuu kwa hiyo alishajiwekea wigo asishitakiwe na hilo tumelishihudia kwenye rada kwani Hosea{msukuma aliwekwa PCCCB amlinde ANDEREA Chenge , Dr. IDRIS RASHID na wenzake wasiende kwa PILATO)
Kijana Feleshi {DPP)aliye na uhusiano wa karibu na Edward Hosea linked to CHENGE alipekua vipengele vya Sheria na sio bahati mbaya alipopelekwa mahakamani alishtakiwa chini ya sheria Kifungu No. 41 ambacho adhabu anayoweza kupewa ni faini ya TSHS.15,000/= au kifungo cha miaka miwili jela na lazima atapigwa faini akale vijisenti kwa amani hiyo ndiyo sheria!!kwa sababu ni mara ya kwanza na yeye ni Mbunge tena mwenye Vijisenti mpaka Ulaya wanamtambua.

Mallya aliyesadikiwa aliendesha gari na hakuwa amelewa wala hakuna aliyemwona akiendesha hilo gari lilomwua marehemu Wangwe alishitakiwa chini ya kifungu No.40 ambacho adhabu yake ni faini na kifungo cha miaka mitatu na amefungwa ila nasikia amekata rufaa.

Sheria inafuatwa kulingana na wewe ni nani ehee!!! Chenge alilewa Polisi chini ya Kivuyo hawakupima kiwango cha ulevi;pili alikuwa hana leseni;tatu gari haikuwa na Bima wala haijalipiwa Road LICENCE na inatembea barabarani for two years wala hakuswekwa lupango kama Mallya!!!!

Nashawishika kuwaambia walalahoi tuungane na Mh. Pinda mtoto wa MKUBWA au mkubwa mwenyewe au Mbunge au Pedege, akitenda kosa ni sharti auwawe papo hapo kwani ukimpekeleka Poilsi inakula kwako tumeshuhudia kuanzia mtoto wa RUPIA aliua baba yake akiwa Katibu mkuu Ikulu akaachiwa , Marehemu Ditto Captain wa JWTZ akitumia bastola yenye silencer kuua dereva mndengereko akapewa dhamana na Kikwete akabariki hilo!! Mungu akachukia akampeleka mwenyewe mbele ya haki!!! Chenge kaua wadada wawili aliokuwa anapeta nao kule Mwanza kaachiwa!!! Mweee!! siingilii mahakama lakini habari ndio hiyo lazima atapigwa faini na waandishi waendelee na njaa zao si mliskia pale Mhakama ya Kinondoni yule Mamaa si alisema mchana kweupee!!!

Alisema marehemu Nyerere!! Haka kanchi kanauka rushwa that was in 1995 je leo baada ya almost 15years kananukaaaaa! tena kimbaa!!!!

Mhache!

Pole sana mdogo wangu!!! Kama sijasahau sana kesi ya Vijisenti iliahirishwa mpaka tarehe 24 April 2009. Maelezo ya mwisho niliyotoa ni hayo hapo juu na hukumu imetajwa si usome!! Ukiona watu wamekaa kimya ina maana wamekubali !!!! Hapa jamii forum ndizo alama za nyakati jifunze!!!!

Mie sijasema kitu kwani ni kuingilia mahakama INAYONUKA rushwa anyway!!! Right or wrong wanoamua mwelekeo wa kesi ni hao wanojifanya prosecutors kumbe ni fix !!! Kama rada ina ushahidi na Edward Hosea mla rushwa No. !!!!!! shit!!!!! amebana nakuambia hatashitakiwa sio Chenge; Sio Rashid!! wala Rostam Aziz.

Mkataba aliopewa Eliezer Feleshi wa kuwa DPP unamkataza kufanya lolote linalowahusu wanamtandao wote pamoja na Malanda wa EPA!!
 
Chenge in the dock over deaths

By AMINA JUMA, 28th April 2010 @ 12:00, Total Comments: 0, Hits: 293

THE Kinondoni Resident Magistrate's Court started hearing a traffic case involving Bariadi West Member of Parliament Andrew Chenge (62) today.

The MP is charged with careless driving. His motor vehicle allegedly knocked a tricycle (Bajaj) and killed two people.

The prosecution side, led by State Attorney Richard Rweyongeza, is expected to parade eleven witnesses in the case -- two of whom testified yesterday. The case was mentioned for the first time in March, last year.

The first witness, Sergeant Solomon, who is a traffic police officer, told the court that he inspected Chenge's motor vehicle (Registration Number T 512 ACD) which was being driven by Chenge himself when the alleged accident occurred.

Sergeant Solomon said that the motor vehicle was damaged during the impact. He told the court that the vehicle got damaged at the front, especially the bonnet, left side indicator, air-conditioner and radiator.

He said that he prepared an inspection report which was handed over to the court as supporting evidence. The second witness, Sergeant Dyego (a traffic police officer), told the court that he inspected the Bajaj tricycle (Registration Number T 736 AXC) and found that it had been knocked from the front. All the seats and other parts of the bodywork were damaged.

He told the court that the rider of the Bajaj, Abdallah Hamis, disappeared immediately after the accident and is still at large. The police are still searching for him.

The defence side, which is led by Advocate Simon Mponda, asked the second witness to explain how the rider of the Bajaj managed to leave the scene of the accident after the accident in which all the seats were heavily damaged.

Sergeant Dyego replied that what he knew was that the rider survived death and disappeared after the accident. The police do not know where he is.

Chenge allegedly committed the offence on March 27, last year, at around 4.30 am along Haile Selassie Road, in Dar es Salaam.

That day, Chenge, who was driving a Toyota Hillux Double Cabin with Registration Number T 512 ACE, allegedly drove recklessly and caused the accident, according to the prosecution.

Apart from allegedly causing the two deaths, Chenge is further accused of causing damage to the Bajaj and driving a motor vehicle without insurance cover on a public road.

The Principal Resident Magistrate, Kwey Rusema, adjourned the case to May 10, this year, whereby more witnesses will give their testimony.

SOURCE: Daily News
 
Huyu Mnyantunzu Vijisenti Chenge,Mungu atamwonyesha nani ni mkubwa zaidi.
Ajabu bado ni mbunge mpaka sasa,hata kesi yake ya Vijisenti sijui imefika wapi.

Shame on me,Shame on You for watching our Tanzania going in this way
 
Chenge atashinda hii kesi kama dereva wa Bajaj hatapatikana! Huyo dereva ndiyo key witness ktk kesi hii.
 
Yale yale ya Zombe, shahidi mkuu kutoweka mpaka leo haonekani. hivi dereva wa Bajaji anaweza ruka pale wakati iko mwendoni tri-cycle?
 
alipopiga za rada tukampa utemi, akagonga na kuua madada wawili waliokuwa kwenye bajaj tukampa cheo cha kuandaa bajeti bungeni, akapiga za escrow tukampa kazi kutuandalia katiba!!

ALIYETUROGA KAFA
 
Back
Top Bottom