Umenikumbusha mbalii
Haya mambo ya sherehe za harusi sitaki tena kujihusisha...
Nilifunzwa enzi zetu shughuli ikowa ya kwenu wale ndugu wa karibu ndo mnaishika sherehe na siku ya shughuli nyie hamshereheki bali mnakuwa wima na macho kuangalia wageni wanapata huduma zote mlizoandaa ukumbini.
Na ndo maana ya vunja kamati, ile sasa sio kila aliyekuwa anakuja kwenye vikao ndo aje kwenye vunja kamati, hapana watakuwa wale ndugu wa karibu waliokuwa wima sherehe nzima kuanzia kupokea wageni, hadi kusafirisha wale waliozima ukumbini na kuhakikisha zawadi zimefika salama kwa maharusi.
Maana ssiku ya sherehe pamoja na kuwa mtakuwa mmependeza ila inawezekana kabisa mkaishia kunywa soda moja au maji moja na saa ingine hata chakula msile.
Busy busy, ila siku ya vunja kamati sasa weeeh hapo ndo mnapiga ulabu na nyama na vyuku kama vyotee.
Miaka kadhaa nyuma ndugu (mabinamu) wakanishirikisha kwenye sherehe kama ndugu wa karibu, aiseeh nikauvaa uhusika nilipiga makitaimu mule ukumbini sina hamu. Nilijitoa hata mziki sikucheza mwisho wa shughuli nikawa hoiii kwa uchovu, sasa hao mabinamu waliniboa.....harusi ya mdogo wao, wao wakaingiza marafiki zao ukumbini naa kukaa kwenye meza kutaka kuhudumiwa.... walikunywa wakalewa hakuna hata ushirikiano kwwnyw kusimamia shughuli....
Nilichukia,nikasema wacha nifanye wajibu wangu ila... hawanioni tenaaa kwenye sherehe zao.
Ndugu mkishikana na mkaelewana hamhitaji floor manager. Kila mtu akae sekta yake na awajibike..
Eeeh sijui nani anifunze kufupisha habari.... nashindwaa....😑