Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 857
- 926
Natumai nyote ni wazima wa afya.
Swala la kuwa Mzee Msuya ni waziri mkuu mstaafu halina utata kwakuwa karibia kila mtanzania anajua
kuwa nchi hii imewahi kuwa na mawaziri wakuu kadhaa ambao kwa sasa ni wastaafu.
Utata unakuja tunapoambiwa mzee Msuya vilevile ni makamu wa kwanza wa rais maana yake nini?!
Kuna wenzetu hasa kile kizazi cha 2000 wameelewa kimakosa kwamba mzee Msuya ndiye wakwanza kushika nafasi ya makamu wa rais wa Tanzania!
Hawa wameelewa kimakosa!.
Maana sahihi ya mzee Msuya kuwa makamu wa kwanza wa rais ni kwamba aliwahi kuwa na cheo au nafasi ya uongozi serikalini baada ya rais inayoitwa MAKAMU WA KWANZA WA RAIS kama ilivyo kwa sasa kwa serikali ya Zanzibar kwamba kuna rais, makamu wa kwanza wa rais na makamu wa pili wa rais na sio kweli kwamba mzee Msuya ndie wa kwanza kushika au kupata cheo hicho cha makamu wa kwanza wa Rais!
Baada ya kulifahamu hilo mimi pia niliingia ndani ya utata na mashaka!.
Mashaka yangu ilikuwa ni je Tanzania iliwahi kuwa na nafasi ya makamu wa pili wa rais kama ilivyo sasa kwa serikali ya Zanzibar?!
Ili kupata majibu hayo nikaanza kufanya utafiti mitandaoni kwa kuangalia hasa watu waliowahi kushika nafasi za makamu wa rais na waziri mkuu.
Utafiti wangu ukanifanya nione kwamba kanuni na taratibu zilizokuwepo baada ya muungano na kabla ya mwaka 1995 ni kwamba endapo rais wa Muungano atatokea Tanzania bara , Rais wa Zanzibar atakuwa na cheo cha pili ambacho ni makamu wa kwanza wa rais wa jamhuri ya muungano na patakuwepo makamu wa pili wa rais wa muungano kutoka bara ambaye pia atakuwa na cheo cha pili ambacho ni waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano.
Na endapo rais wa jamhuri ya muungano atatokea Zanzibar basi yeye rais wa Zanzibar atakuwa na cheo cha pili ambacho ni MAKAMU WA PILI wa rais wa jamhuri ya muungano na MAKAMU WA KWANZA wa muungano atatokea Tanzania bara ambapo pia atakuwa na cheo cha pili ambacho ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwahiyo katika serikali ya mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anatokea Tanzania bara utawala ulikuwa hivi:.
1️⃣ Rais wa jamhuri ya muungano ambaye anatokea Tanzania bara.
2️⃣Makamu wa kwanza wa rais wa jamhuri ya muungano ambaye pia ni rais wa Zanzibar.
3️⃣ Makamu wa pili wa rais wa jamhuri ya muungano ambaye pia ni waziri mkuu wa jamhuri ya muungano.
Baada ya mwalimu Nyerere kung'atuka na kumuachia serikali mzee Mwinyi (Rukhsa ) ambaye alikuwa anatokea Zanzibar utawala ukawa hivi :
1️⃣ Rais wa jamhuri ya muungano ambaye anatokea Zanzibar.
2️⃣ Makamu wa kwanza wa jamhuri ya muungano ambaye pia ni waziri mkuu wajamhuri ya muungano kutokea bara.
3️⃣ Makamu wa pili wa rais wa jamhuri ya muungano ambaye pia ni Rais wa Zanzibar.
MAKAMU WA KWANZA NA WA PILI WA RAIS WA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA.
1️⃣ Rais = J. K . Nyerere.
2️⃣ Makamu wa kwanza wa rais.
1.Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume
1964 - 1972.
2. Rais wa Zanzibar Aboud Jumbe Mwinyi
1972 - 1984
3. Rais wa Zanzibar. Ally Hassan Mwinyi ( Mzee Rukhsa)
1984 - 1985
3️⃣Makamu wa pili wa rais (serikali ya awamu ya kwanza)
1.Waziri mkuu Rashid Mfaume Kawawa 1964 - 1977.
( Kuanzia mwaka 1977 hadi 1985 ilipoingia serikali ya awamu ya pili hapakuwa na makamu wa pili wa rais )
MAKAMU WA KWANZA NA WA PILI WA RAIS KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA PILI.
1️⃣ Rais = Ally Hassan Mwinyi ( Rukhsa )
2️⃣ Makamu wa kwanza wa rais=
1. Waziri mkuu Joseph Sinde Warioba.
1985 - 1990.
2. Waziri mkuu John Samweli Malecela
1990 - 1994.
3. Waziri mkuu Cleopa David Msuya
1994 - 1995.
3️⃣Makamu wa pili wa rais ( serikali ya awamu ya pili )
1.Rais wa Zanzibar Sheikh Idris Abdul wakil. 1985 - 1990.
2. ( Kulingana na makala ya gazeti la MWANANCHI la tarehe 22 September 2015 pia 16 March 2021 )
Rais wa Zanzibar Salmin Amour Juma ( Komandoo )
1990 - 1995.
Soma pia TANZIA - Mzee David Cleopa Msuya afariki Dunia akipatiwa matibabu hospitali ya Mzena