Cheo ni dhamana - Viongozi lindeni heshima ya future yenu

Pongezi kwa wateule wote,
mara baada ya kiapo wanapaswa wachape kazi kwa speed na weledi.
Watanzania wengi tunapenda kuona Watendaji wanafuatilia miradi ya serikali kwa karibu.
hatupendi kuona viongozi wanakaa ofisini tu.
Mfano, Prof: Mbarawa ni mfuatiliaji mzuri ila sio mkali hivyo ili afanikiwe ni lazima awe mkali pale inapo bidi.
Makamba ni mfuatiliaji mzuri ila apunguze ushikaji kazini apige kazi, nishati ni nguzo ya uchumi wa Taifa.
Kijaji ni mpambanaji mzuri sana pia ni mkali hapendi masihara awapo kazini.
Mama Tax ni mweledi tunategemea maboresho mazuri zaidi.
 
Mkuu, naona umeongea kimafumbofumbo?
Ila kuna jamaa walibebwabebwa sana! Sijui itakuwaje?
Hivi ni rahisi kurudisha humbleness iliyopotezwa kwa sababu ya godfather?
 
Prof. Mbarawa tunakuomba acha upole, kuwa mkali.
tunakufahamu wewe ni mfuatiliaji mzuri sana ila tatizo una kaupole, wapigaji na wabadhirifu huwa wanapenda sana kusimamiwa na mtu mpole ili wapate namna ya kupiga vizuri.
hivyo tunakuomba ongeza ukali ili miradi isonge kwa kasi.
 
Umepata bahati ya kuteuliwa na Mhe. Rais ktk nafasi yoyote ile kwa nini tena uote mapembe badala ya kuwatumikia wananchi.?
mimi ningepata nafasi ya kuteuliwa na Rais ktk nafasi yoyote ile ningetumika bila kuchoka.
 
Congratulations Mr. Mbarawa. Sincerely!! Welcome back again! You sincerely fit to the post. I do remember your visits in Kigoma. Welcome again.
 
Heri ya mwaka mpya na mambo mapya wakuu?

Naimani kwa uwezo wake Mungu tuliobahatika kuupokea tumeupokea na wenzetu walioupokea wakiwa vitandani tuwaombee kwa Mungu awafanyie unafuu warejee katika khali zao.

Na waliotangulia mbele za haki ya bila kuuona mwaka mpya tuwaombee wapumzike wanapostahili.

Niwakumbushe tu kama kichwa cha habari kinavyosema cheo ni dhamana tukitumie vzr na tuishi na watu vzr na tuwaheshimu wale tunaowaongoza maana bila wao tusingelipewa vyeo tulivyonavyo , cheo isiwezi sehemu ya kumchapia mwenzio bali iwe sehemu yakuelekeza kwa hekima na busara .

Niwatakie Kheri Ya Mwaka Mpya Na Mambo Mapya.
 
Uongozi siyo Ubabe: Ndugai alimpiga mwenzie bakora, Jafo alimkemea Injinia hadi akazirai, Ngeleja naye alimtesa mlinzi but Leo wako wapi?

Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba Cheo ni dhamana

Usitumie Cheo chako kama silaha ya kutweza UTU wa watu wengine

J4 Mungu akubariki!
 
Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba Cheo ni dhamana

Usitumie Cheo chako kama silaha ya kutweza UTU wa watu wengine

J4 Mungu akubariki!
Magufuli aliwatesa wengi, aliwaua wengi, aliwapoteza wengi, aliwadhulumu wengi, naomba naye umuweke kwenye list. Usiwe na selective "prosectution"
J4 njema Mungu wa Mbinguni (siyo wa dunia kama magufuli) akubariki kwa thread nzuri.
 
Samia nae yatamkuta tu kwa jinsi anavyowafanyia Watanzania.
 
Huo usemi uliishia kwa Hayati Nyerere,hauko tena,na sa hivi cheo si dhamana tena.
Rais Samia Suluhu bado anautumia anakwambia yeye ni mtumishi wako anafanya kile unapenda wewe mtanzania na si vinginevyo kwasababu wewe ndio boss wake (muajiri)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…