cheti cha kifo

cheti cha kifo

Finder boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
608
Reaction score
150
Nilifiwa na baba yangu mwaka 2007 ila kwa bahati mbaya hakukuwa na mtu wa kufuatilia cheti cha kifo, sasa nimekua na ninataka kufuatilia cheti icho. Je nitakipata wapi? Na ni hatua gani napaswa kuzifuata ili nipate cheti icho?. Naombeni msaada wenu
 
Tafuta Muktasari wa KIkao cha familia kukuthibitisha kuwa mfuatiliaji, Nenda serikali za Mitaa wakupe barua ya kwenda RITA
 
Pia ni vizuri kufuatilia kibali cha mazishi kama kipo. Ikiwa alifia hospitali, basi yumkini mwanafamilia mmoja alipewa hicho kibali.
 
Ndugu, nenda RITA au ofisi ya mkuu wa wilaya ile ambayo kifo cha marehemu baba yako kilitokea, utapata kuandikisha cheti cha kifo kilichocheleweshwa kuandikisha ila utatozwa ada kidogo sana (hela ndogo kama ya lunch tu)....utapata na risiti ya hiyo hela utakayotoa, sio rushwa. cheti cha kifo ni muhimu sana katika kugawa mirathi na kushugulikia mambo mbalimbali kama vile mafao ya marehemu, insurance tec. nakushauri wewe na watuw engine pia, download copy of this book hapa chini, its just a cover, kisome mle ndani, nimeliweka pia hili jambo. you will not regret it. karibu sana.
View attachment 97972
View attachment 97972
View attachment 97972
 
Pia ni vizuri kufuatilia kibali cha mazishi kama kipo. Ikiwa alifia hospitali, basi yumkini mwanafamilia mmoja alipewa hicho kibali.
Yeah, kama una kibali cha mazishi, hiyo death certificate unaipata chap chap
 
Back
Top Bottom