Cheti gani cha ndoa kinachotumika kwenye uhamisho serikalini?

NOLDJAY

Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
7
Reaction score
0
:A S 12:Naombeni msaada Wenu wana JF, mimi natararajia kufunga ndoa kanisani mwez wa 12 mwaka huu. swali ni je cheti cha ndoa nitakachopata kanisani kinatambuliwa na serikali kwenye uhamisho wa mwanamke kumfuata mume? Maana wengine wanasema mpaka cha bomani sasa sijajua tofauti hapo. Nahitaji msaada wenu wana JF:A S 12:
 
Utapewa vyote viwili. Cha kanisani na cha Serikali. Tulia usiwe na shaka.
 
Cheti cha ndoa kipo kimoja tu, na vyeti hivi vinatolewa na serikali ya JMT, ufunge ndoa ya aina yeyote ile cheti kitatolewa kimoaja ila zinakuwa copy mbili ya mke na mme. Huu ndo ufahamu wangu mimi nimefunga ndoa ya kanisa katoliki na nimepewa cheti cha serikali, kanisa langu limeridhia kutumia cheti hiki kama hati ya ndoa.
 
Ni kweli vyeti vya ndoa ni document ya kisheria inayotolewa na serikali. Wachungaji, masheikh na wakuu wa wilaya wanaitwa wasajili wa ndoa. Wananunua kitabu na kuweka records. Kuna baadhi ya makanisa wanatoa vyeti vya kanisa. Ila vinakuwa havina logo ya serikali ya jamhuri. Kazini unapeleka kile chenye logo ya jamhuri.

Hongera kwa kupata mwenza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…