Tukio la tuzo za kili limeshapita,lakini vumbi lake bado linatimka,na chafya zinazidi kuongezeka.Kama inavyokuwa miaka yote lawama zimeendelea kuwepo,kunyosheana vidole,vijembe,kujigamba n.k kupo pale pale.
Midahalo imekuwa mingi sana lakini huu wa Ali kiba kuchukua tuzo nyingi umekolezwa zaidi.Umekolezwa kwa sababu ya uwepo wa timu mbili zinazokinzana kwa sasa,timu kiba na timu Diamond.Makala yangu imelenga kuchokonoa jipu hili.
Kuna watu wanao amini kuwa Ali kiba alistahili kuchukua tuzo alizopata na wengine wanahoji kwanini diamond apate tuzo chache licha ya viashiria vingi vya kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimataifa.
Kwa mtazamo wangu Ali Kiba alistahili kuchukua tuzo alizopata kutokana na vigezo vifuatavyo;
Kwanza kabisa Ali kiba alistahili kushinda kwa kuwa aliingia kwenye category zile na yeyote aliyeingia kwenye category husika ana haki ya kushinda tuzo husika.Kama kulikuwa na room ya kulalamikia ushindi wa Ali kiba katika category yeyote basi malalamiko hayo yangeanzia wakati jina lake limeingizwa kwenye category.
Pili,Ali kiba alifanya kampeni ya kuomba kura na alipata marafiki wengi wenye ushawishi waliojitokeza kumuombea kura kwa mashabiki mfano Wema Sepetu,Jokate,Abdu kiba na wengineo.
Tatu,Ali kiba ni mwanamuziki wa muda mrefu,anajua kuimba,ana sauti nzuri na fundi wa kuandika nyimbo hivyo siona shaka kwa mtu wa hulka hiyo kutunukiwa tuzo nyingi ambazo hata 'msanii 20%' alizipata miaka michache nyuma.
Diamond siyo mwanamuziki mbaya,wala kukosa tuzo hakumaanishi kuwa diamond ni mbovu kuliko kiba,ikumbukwe kwamba hizi tuzo hutolewa kwa wasanii waliofanya vizuri katika mwaka husika hivyo kama mashabiki wameona kuwa kwa mwaka uliopita Ali kiba ndio amefanya vizuri kupitia wimbo wake wa Mwana basi maamuzi yao yaheshimiwe na tusubiri mchakato mwaka ujao.
Diamond hakujihusisha sana na upigaji kampeni hivyo kwa tuzo mbili alizopata bado ni ishara kuwa anapendwa na kukubalika na mashabiki.
Kufanya vizuri kimataifa hakumpi Diamond guarantee ya kuchukua tuzo za ndani kwa kuwa mbali na sifa nyingine nyingi alizokuwa nazo Diamond Video zake nzuri ndio zimemfanya apae kimataifa, Watanzania watam-judge Diamond kwa kuangalia zadi ya video anazotoa.
Diamond ni mwanamuziki mkubwa kwa sasa barani Afrika,anafanya vizuri na kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi hastahili kubezwa,kuchukiwa,kushushwa wala kufanyiwa fitina na mtanzania wa "timu" yeyote.
Ali kiba ana potential ya kuja kuwa mwanauziki mkubwa,mkubwa kuliko anavyoweza kujitathmini,ushindani uliojitokeza baina yake na diamond unaonekana kumwamsha kifikra,lakini bado hajafanya yote aliyotakiwa kuyafanya,naamini[kama anajielewa] akitiririsha yote yaliyokuwa kwenye locker lake tutakuwa tunaongelea balaa lingine.