Chicken coming home to roosting place

Swali langu ni kwamba,lin maisha yaliwahi kuwa nafuu???

Hata kipind hiko Magufuli yupo si bado mlikuwa mnasema vyuma vimekaza?
Slogan ya vyuma kukaza wengine tunaweza kusema ilikuwa ni slogan ya kimkakati kutoka kwa wale vibaka waliobanwa na Magu.

Tuliobaki tulishuhudia kipindi kirefu sana cha umeme kutokatikakatika na stability ya mfumuko wa bei kuliko kipindi chochote miaka ya hivi karibuni.

Anyway, basi tunaweza kuassume kwamba mfuko wa mbolea kutoka 50K hadi 150K ndani ya mwaka mmoja ni jambo tu la kawaida.
 

Tukiacha ushabiki pembeni,hatuwez kujisahaulisha ugum wa maisha uliokawepo kipindi Cha Magufuli ulivyokawa unakatisha tamaa,

Kama vile ulivyokawa kwa Magufuli ndivyo hivyo hivyo ulivyo kwa Samia,Plus kwa sasa Kuna janga lingine la Vita,kikubwa ni kuitaka SERIKALI iangalie strategic measures za kufanya subisidy katika hili la mafuta Ili liweze kusaidia kucontrol inflation
 
Inshu ya mfumuko wa bei ni zaidi ya kile kinachoendelea huko duniani na haiwezi kushughulikiwa kwa simple subsidy. Kuna uhusiano gani kati ya kupanda kwa bei za mbolea inayozalishwa Minjingu na vita ya Ukraine?

Mfanyabiashara akishangundua kuna loophole sehemu katika mifumo ya serikali ataitumia kisawasawa kutengeneza super-profit. Hapa kwetu wameshajua wapi kuna kaupenyo na wanakatumia effectively.
 
Swali langu ni kwamba,lin maisha yaliwahi kuwa nafuu???

Hata kipind hiko Magufuli yupo si bado mlikuwa mnasema vyuma vimekaza?
Watanzania ni wasahalifu Sana. Wanasahau hali ilikua ngumu tokea kipindi cha Magufuli na mbaya zaidi ukihoji tu unakutana na wasiojulikana.
Yule mzee hafai kabisa
 
Hii bado ni awamu ya 5 na mama alisema yeye na Magufuli ni wamoja.
 
Samia ni incompetent...Mimi uwa namuonea huruma tu baada ya miaka mitatu ijayo nchi itakuwa kwenye hali gani.
 
Nilijua umeandika cha maana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazanzibar huwa wanatabia ya uvivu hilo linajulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nataka ku address hii habari ya kwamba Magufuli ni chanzo. Mimi si mtetezi wa Magufuli, hivyo nisisomeke kama namtetea Magufuli.

Nataka kuonesha mizizi ya tatizo ilivyo mirefu kuliko Magufuli.

Ukiisoma historia ya Tanzania vizuri, utagundua kwamba hakuna kipya alichofanya Magufuli ambacho hakijafanywa awali huko kuanzia serikali ya Nyerere.

Kuanzia kukandamiza wapinzani mpaka white elephant megaprojects.

Tofauti kubwa ni kwamba utawala kama wa Nyerere ulijaribu kufanya mambo mengi kijanja na kisheria, Magufuli alifanya kihuni na kibabe.

Magufuli kaminya wapinzani? Nyerere alifuta vyama vingi kabisa. Vijana wengine hawajui kwamba Tanganyika ilikuwa na vyama vingi na kulikuwa na wapinzani kina Christopher Kassanga Tumbo na Joseph Kassela Bantu, Nyerere aliwazima na wengine walikatazwa kutoka vijijini kwao.

Magufuli aliingilia Bureau de Changes? Nyerere alitaifisha mabenki kabisa.

Magufuli kaingilia biashara ya korosho?
Nyerere alitaifisha mashamba kabisa.

Magufuli alitukana wapinzani? Nyerere aliwaita malaya kabisa.

Magufuli kaiba uchaguzi? Nyerere ndiye alikuwa mastermind wa kubadili chaguzi Zanzibar as far back as 1985 kwenye enzi za chama kimoja. Uchaguzi wa Ndiyo/ Hapananule wa kushindanishwa na kivuli Idris Abdul Wakil alishindwa urais Zanzibar lakini CCM ya Nyerere ikabadili matokeo.

So alichofanya Magufuli ni muendelezo wa kilichoanza miaka mingi sana utawala wa Nyerere, sema Magufuli kafanya kishamba na kibabe, Nyerere alifanya kijanja na kisomi.

Soma kitabu cha Paul Bjerk "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania 1960-1964"
 
Hizo ndege alizonunua kwa cash 💴 bila auditing alinunulia familia yake? Si ameziacha kwa JAMHURI ya MUUNGANO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…