Chid benz amwaga machozi clouds alivyokuwa anaelezea story ya diamond kabla hajakuwa star

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689

Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa.
Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake.

Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya 'Mpaka Kuche' aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi.

Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali.

Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri.
"Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa," alikumbushia Chidi.
 
Seems Kila mtu anajaribu awezavyo kupata kick kupitia jina diamond sasa. Jamaa kawashika hakika

Nasikia Kiba nae kasanda kaanza kutafuta uwezekano wa kufanya kazi na platinumz baada ya nyimbo zake alizotoa kuishi muda mfupi hewani
 
maneno ya mkosaaaji,na hao klaudi efuem wanasema wanasambaza upendo wakati wanasambaza ngono!
Acheni dhambi nyie,mimi ningekuwa paroko st.peters oysterbay singempa ekarist Ruge,ni muuaji,watu wametorosha madenti hapa dar wameenda kuwagegeda tanga eti sambaza upendo!
Mungu yupo mtalipa kwa machozi ya damu
 
kweli UMEGUSWA
 
Seems Kila mtu anajaribu awezavyo kupata kick kupitia jina diamond sasa. Jamaa kawashika hakika

Nasikia Kiba nae kasanda kaanza kutafuta uwezekano wa kufanya kazi na platinumz baada ya nyimbo zake alizotoa kuishi muda mfupi hewani
Mwana Daresalaame ndio wimbo wa Taifa wewe sijui upo sayari gani?
 
Seems Kila mtu anajaribu awezavyo kupata kick kupitia jina diamond sasa. Jamaa kawashika hakika

Nasikia Kiba nae kasanda kaanza kutafuta uwezekano wa kufanya kazi na platinumz baada ya nyimbo zake alizotoa kuishi muda mfupi hewani

mkuu hivi unajua nani hataki kushirikiana na mwenzake katika kutoa nyimbo ?
muulize ommy dimpoz
 
You are miss informed..
Alikiba ndyo hataki kufanya collabo na diamond..
 
Kitafuta kikii tu...

HipHop ni kama kamari tu.
 
Sembe inaongea....ndo manini sasa
mi mwenyewe sijaelewa anachoongea zaidizaidi naona anabiringisha....
dbp.jpg
 
Ovyooo......keshaanza kua mtabiri sasa eeh? USO umemsawajikaaaaa....sijui kakutwa na yepi....

"The truth is hard to swallow when you're choking on your pride."
 
You are miss informed..
Alikiba ndyo hataki kufanya collabo na diamond..

mkuu hivi unajua nani hataki kushirikiana na mwenzake katika kutoa nyimbo ?
muulize ommy dimpoz

Kiba alijidai kukataa ila sasa anaomba kufanya kazi na Diamond. Namaanisha ninachoongea na si vinginevyo

Kila msanii anawaza kufanya kazi na diamond ili watoboe kwa jina la jamaa. Kwa last interview Kiba kafanya kakiri uhitaji wa kufanya kazi na diamond. Realistically Kiba anamuhitaji zaidi diamond kuliko diamond anavyomuhitaji Kiba
 
Seems Kila mtu anajaribu awezavyo kupata kick kupitia jina diamond sasa. Jamaa kawashika hakika

Nasikia Kiba nae kasanda kaanza kutafuta uwezekano wa kufanya kazi na platinumz baada ya nyimbo zake alizotoa kuishi muda mfupi hewani

Njaa inapohamia kichwani akili huhamia tumboni. Naona haya ni mawazo ya tumbo lako.
 
Back
Top Bottom