Chid Benz kapona tayari, huu ndio muonekano wake mpya

Chid Benz kapona tayari, huu ndio muonekano wake mpya

Hadi anakumbuka aliyoyafanya wakati yuko ndwiii, kumbe alikuwa na kumbukumbu nzuri. Ila watu wanataka kumtumia harakaharaka ili wapige pesa. Mbona mnaweza kumuacha apone vizuri ili afanye vizuri zaidi?
 
Msanii wa kizazi kipya mwenye rekodi ya kupatwa na misuko suko ya madwa ya kulevya amepata nafuu na sasa ameingia studio kutoa ngoma aliyomshirikisha Mr Blue na Matonya kabla ya kuumwa, na sasa atafanya ngoma nyingine hayo yamesemwa na Rash Don



Kwa jicho langu Kali lililotukuka kwa muonekano huo wa Chidy Benz naona bado hajapona tena kabisa na pengine anahitaji kuendelea kuwa rehab hata kwa mwaka mmoja zaidi au hata miwili ndipo arudi kuwa vizuri. Uponyaji wa utumiaji wa Ngada huwa hauwi haraka hivi Mkuu na usijidanganye wala picha zisikudanganye. Hivi kama T.I.D bado Ngada haijamuisha Kichwani ndiyo itakuwa kwa Chid Benz? Sasa nikusaidie tu kukufahamisha labda usichokijua ni kwamba kuna Watu fulani fulani Wajanja wa Mjini ( Wazee wa Fursa Media ) njia panda ya Coca Cola Mikocheni wanalazimisha Jamaa aonekane kuwa kapona kabisa matumizi ya Ngada ( Unga / Dawa za Kulevya ) ili Yeye pamoja na Ray C ( Rehema Chalamila ) waandaliwe bonge la show ambalo litaratibiwa Kiutaalam na kupewa Promotion ya kutosha ili tu hao Wajanja wa mjini wapige Hela / Pesa / Mtonyo kupitia wao. Na inasemekana hao Jamaa watakuwa wanazunguka nao katika baadhi ya Mikoa mikubwa nchini Tanzania kwa Kigezo cha kuwaelimisha Watanzania athari za matumizi ya dawa za kulevya. Itunze hii post yangu Mkuu kwani nina uhakika na nilichokiandika hapa kuwa very soon kinaenda kutokea. Hii ndiyo Tanzania bhana!
 
Watu ambao wameamua kumsaidia Chid hawako sawa kabisa ivi kuna sababu gani ya kumrudisha kwa haraka then mnapeleka studio afanye joint hata kabla hajajifanyia tathimini ya kina yeye mwenyewe huo muziki ndio chanzo cha mabalaa yake,utasikia kesho ana show Kinondoni hapo ndipo ndugu zake katika unga hawatokubali apite bila kuonja duh uyu jamaa wanaomsaidia ndio watakao mpoteza.
umesema kweli,by the way huyu mshkaji ana hip hop yake yani iko safi,kusema kweli asingefanya usengerema Nay angekua analima kwao huko,hata darasa sijui angeimba wapi,kuna siku nilipiga beat zake tu mfululizo mahali watu walisimama,mwisho wanauliz huyu mnymwezi gani nikaapa picha yuko haire walichoka
 
Ishu ya madawa huponi faster namna hiyo.. tuipe muda tuone atafika wapi
 
Back
Top Bottom