Chid benz: Naacha kuvuta unga!

Chid benz: Naacha kuvuta unga!

Iyokopokomayoko

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2011
Posts
1,785
Reaction score
442
Stori: Shakoor Jongo
Rapa maarufu Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz' ameibuka na kueleza kwamba alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu lakini sasa ameamua kuacha baada ya kubaini kuna madhara makubwa.

Akizungumza kupitia Kipindi cha XXL cha Clouds Radio juzikati, Chid Benz alisema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya kushtukia kuwa alikoingia siko ndipo alikwenda kwenye matatibu nchini Kenya na hatimaye kufanikiwa kujitoa kwenye orodha ya mastaa wanaobwia kilevi hicho.

"Nilimwambia mama yangu kuwa lazima nitibiwe, nimefanya hivyo bila kwenda ‘rehab' wala kunywa dawa, sasa niko fresh, niko healthy (nina afya), nakula vizuri, nafikiria vizuri na sasa nimetulia," alisema Chid Benz na kuongeza:

Nilianza kutumia unga miaka mingi iliyopita lakini ilikuwa ni vigumu watu kujua kwa kuwa nilikuwa nakula vizuri, nafanya mazoezi, naoga kwa hiyo nilipokuwa nikitumia yalikuwa hayanitibui ila yananijaza tu chuki na ule unomanoma."
Gazeti hili linampongeza Chid Benz kwa uamuzi huo na kuwataka wengine waige mfano wake.


Chanzo: Global Publishers
 
Sawa kama kaacha ila asaidie kuonyesha alikokuwa anazipata.....
 
Ndio maana hii biashara imeshamiri nchini, kumbe mateja yapo ya kutosha.!
 
Huyu nae lazima ahojiwe na aeleze vizuri, ni wapi alikomficha mjinga mwenzie Mangungo, asilete stori zake za ujingaujinga hapa, mbona alipoanza kuwa nyoka hakwenda kutangaza huko sijui kwenye redio au gazetini, hawa si watu wa kuwachekea kabisa!
 
Ehee na aliekuwa anakuuzia nani mr chid

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hana lolote huyo acha wanyamwezi wamle ndo ataacha
 
huyu itakua aliwahi kujaribu unga mara moja au mbili? utumie unga kwa miaka halafu uje kuuacha kwa kwenda kenya tu..!?
 
Chidi why uache...endelea bwana kwani hatuoni umuhimu wako hapa Tanzania.
 
Ningemuona mjanja kama angeendelea kuvuta
 
wanafanya sembe fashion mwisho wa siku wanaFamilia wao ndio wanahangaika ! Ama kweli Mtafuta Janga hula na nduguze!
 
Back
Top Bottom