warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
RAPA mwenye jina kubwa katika Bongo Fleva , Rashid Makwiro maarufu kama Chid Benz, amekiri kutoa machozi wakati wa mahojiano redioni baada ya kupatwa na hisia kali , akikumbuka mambo mbalimbali ya maisha.
"Nilikuwa namzungumzia Diamond, alinikumbusha mambo mengi, ni mchapakazi, anajituma na amejipanga, anajua alikotoka na anathamini alipopitia, nikajikuta nimepatwa na ' emotions ' zilizonitoa machozi, " alisema msanii huyo aliyetoa kazi mpya hivi karibuni.
Wimbo huo mpya unaokwenda kwa jina la Mpaka Kuchee, ameufanya baada ya kukaa kimya kwa muda wa mwaka mmoja , kiasi cha kuleta hisia kuwa huenda amekwisha makali yake.
Kibao hicho amewashirikisha wakali wengine, mkongwe AY na msanii aliye juu kwa sasa, Nasibu Abdul ' Diamond '.