Chidi Benz asimulia ilivyokuwa hadi kukamatwa na dawa za kulevya Airport

Chidi Benz asimulia ilivyokuwa hadi kukamatwa na dawa za kulevya Airport

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
10711083_1062715290409555_7336867001440902865_n.jpg


Rashid Makwiro a.k.a Chidi Benz ambaye ameachiliwa kwa dhamana Jumatano wiki hii, amesimulia jinsi ilivyokuwa hadi kukamatwa Ijumaa iliyopita Oct.24 na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere.

Chidi alizungumza na Soudy Brown kupitia So So Fresh ya Clouds FM jana.

"Sikuwaambia natumia, niliwaambia dawa ambazo nilikuwa niko nazo lazima nitakuwa nimeconfuse kipindi ambacho natumia nilikuwa ofcoz naweka weka naficha ficha kwenye nguo nguo zangu na nini, so nimewambia maybe kwasababu hiyo nguo sijawahi vaa ndio mara ya kwanza…huwa naweka mashati kadhaa nayatundika tu hivi yako kama kumi kumi na tano, huwa nikivaa najua hili nasafiri nalo au nazunguka tu leo round za town baadae nikilivua nalitupa tu si unajua sisi mara nyingi nguo ukivaa unakuwa unavaa mara moja labda hivyo. So nahisi lazima ile dawa nilikuwa nimeiweka labda niliiweka au nimeficha coz nilikuwa naweza nikachukua hivi enzi zile sitaki mtu aone na nini naiweka kwenye mfuko naiacha hapo na hilo shati sijawahi vaa ndo nimelivaa juzi. " alisema Chidi Benz.

"Shetta alinipigia simu akaniambia tunaondoka leo nikamwambia ooh yeah? Ooh yeah leo fasta, na mimi sasa hivi nakaa Tegeta unajua, so nikachukua lile shati fasta sio la kupiga pasi ni kama hili nililovaa hapa nikalichukua tu nikalipiga na jeans hivyo. Nikaenda zangu airport, niko airport nikamwambia Shetta namtania tu hivyo namwambia mdogo wangu nimebeba mambo nimebeba mambo [kicheko], nimebeba mambo kibao yale mabegi yamejaa yote haya yote mabegi sina nguo wala viatu wala nini hapa nina mambo tu like namtania unajua, lakini sasa nafika pale nasachiwa ndo nakutana na hiyo dawa".

Aliendelea,

"Imagine nimekutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto unajua si kama nimeficha au nimefanya nini. Of course kila mtu anaongea cha kwake hamna yule muongo atakuwa hivi hamna mteja yule of course, so saivi lazima nikubali kwa kila mtu anachokiongea as long kwamba watu walikuwa hawasaidii chochote time ambayo sijakamatwa au sijakutwa hamna kitu chochote walikuwa mtu nasaidiwa au naambiwa kwahiyo naona kawaida tu.

Lakini si kitu nimepanga si kitu nilikuwa nimeplan unajua nimekutwa nayo mimi mwenyewe ndio nimejisachi, si yeye sijakamatwa mimi mwenyewe nimejisachi nimezitoa kushoto kulikuwa na pesa kulia pesa kushoto pesa tena akaniambia we pesa pesa akaniambia hapa mfukoni juu kuna nini, nikamwambia hii I think ni uchafu uchafu tu natoa hivi nakuta vidude kama kadhaa hivi naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona akaniambia bwana hii nini nikamwambia hii…dawa but sijui imekuaje na mimi pale kidogo kibinaadam nilikuwa kama kidogo akili imeniruka kuja kugundua kwamba ile ni dawa na nimeitoa mwenyewe unajua…

Yaani kwanza nakwambia kwasababu hata yeye wakati natoa hizo pesa nilikuwa kama namtania yule jamaa ananiambia mfuko wa nyuma namwambia hizi pesa huku pesa, hii karatasi yangu ya mashairi nataka niandike, hii huku pesa akaniambia na hapa juu nikamwambia hapo juu hamna kitu ni uchafu uchafu tu, hee natoa hivi nakutana na kimkanda unajua so like kama nilipigwa na butwaa hivi unajua."

Chidi alisema alijaribu kuwaomba wana usalama wamuelewe na kumsamehe lakini ilishindikana.

"Nikajaribu kuwaomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikuwa natumia hizi vitu but nikaachana nazo, so wakati naachana nazo ofcoz zamani nilikuwa sio mtu wa kununua kimoja kimoja nilikuwa nanunua labda kadhaa unajua so navyohisi labda siku nilizichomeka kwenye kamfuko haka ka juu wa shati nikaziweka hapa nimesahau nguo nimeivaa tu ghafla nimesahau kiukweli, so please kama mnaweza kunielewa mkanisamehe please, hakuna ninachosafirisha hakuna nini mabegi yangu haya hapa mnaweza mkanisachi nisachini kote, wakasachi kila begi kila kitu hakuna kitu sina kitu kingine, nilikuwa na spika nilikuwa na viatu nilikuwa na nguo done." alimaliza Chidi Benz

Kesi yake imepangwa kusikilizwa tena November 11.


Chanzo:Bongo5.com
 
Chid poda itakupoteza kwenye ramani ya dunia achana na hayo mangada.
 
Madawa ya kulevya yameshamuathiri akili ya huyu msanii amekua hana akili kabisa.
 
Duh....Ina maana basi Chidi akiishi Mererani atakuwa anakuta Tanzanite mfukoni...sasa siju anangoja nini asijisogeze maeneo, ageuke Bakhresa au Mengi wa fasta fasta.
 
Huyu nae amehojiwa na Mtu ambaye hajui kuuliza maswali ya Msingi! Ina maana na vifaa vile vyote navyo vilikuwa kwenye shati siku zote? Na Misokoto yote ya bangi?
 
Sasa ameongea nini?Mimi sielewi hata kidogo...
Jamaa nilivyomuona sikujua kama ndie yeye kaisha vibaya mno
 
Mi naona anajikatia roho tu...waanze kuandaa eneo pale ilala makaburini tutamzika siku sio nyingi huyu!
 
come on people, someone must know something
 
Kila anavyoukataa ukweli ndivyo anavyojiongezea tatizo duh Chid bado yuko gizani na anaamini kua wa-Tz wanaamini pia kaacha ngada ni mwendawazimu kweli.
 
Mi naona anajikatia roho tu...waanze kuandaa eneo pale ilala makaburini tutamzika siku sio nyingi huyu!

mim namtakia maisha marefu maana mambo ya kuanza michango ni ishu tena nyingine
 
Tumuonee huruma sio kumsema vibaya..km angekuwa mwanao au baba yako ungemkashifu?..Huyu msanii apate mshauri mzuri aanze rihab insha allah naamin One day Atapona..

hakuna alie msafi...kuna uteja wavitu vingi kuna wengne humu nimateja wawanawake miteja ya pombe mxxxiu
 
Dah! Kwa stage alofikia bora aache maana hiyo stage alofikia naijua vizuri,wanaokaa nae wamshauri aache.Nimemaliza
 
Back
Top Bottom