Chief Godlove kaumbuka kudanganya gari lake Maybach ni million 800

Chief Godlove kaumbuka kudanganya gari lake Maybach ni million 800

loose Nut

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
2,887
Reaction score
6,657
Tajiri kijana kwenye social media mwenye kujikuza sana Chief Godlove kaumbuka tena baada ya bingwa wa magari used kuonesha gari la Mercedes Maybach analiuza kwa shiling million 40.

Kumbuka gari hilo linalouzwa linafanana kila kitu na maybach ya Chief godlove aliyotudanganya alinunua million 800.

Chief godlove mwenye tabia ya uwongo uwongo kwa kutafuta sifa zembe na za kijinga kujisifia ni tajiri alishawahi kudanganya buti la shilingi elfu 45 analovaa ni alinunua USD 3000.

Aidha wanoko wanathibisha hizo gari zote anazoringia na kunyima watu usingizi siyo zake bali ni ile crown anayotamba ni ya kubeba mbwa wake ndio anayomiliki kihalali.



Source: mimi mkuu wa jopo la wambea JF

adriz de mbusii
 
Pambaneni na maisha yenu vijana, achaneni na mambo ya wengine.
Mkuu,

Kwenye saikolojia kuna anxieties nyingi sana. Kuna status anxiety, kuna poverty anxiety.

Kuna watu wamekulia kwenye umasikini kupata gari kwao ni ndoto.

Wakati mimi nilipokuwa na miaka 14 nilisoma kwenye kitabu cha baba yangu kinaitwa "Swim With The Sharks Without Being Eaten Alive : Outsell, Outmanage, Outmotivate, and Outnegotiate Your Competition" cha Harvey B. Mackay.

Kitabu kina mambo mengi sana, yameandkwa kifupifupi na kirahisi kusoma, hata mimi nikaweza kupata vitu.

Kitu kimoja alichoandika ni kwamba, nunua nyumba za bei kubwa na magari ya bei ndogo. Kwa sababu magari yanashuka thamani na real estate inapanda thamani.

Sasa kama ushaondoa ulimbukeni wa kupanda mabenzi na ma Range Rovr tangu utotoni, hata ukinunua ukubwani unanunua kwa kupata usafiri wenye standrd fulani tu, si kwa poverty anxiety na status anxiety ya kujionesha kwa watu.

Wabongo wengi wapo katika status anxiety na poverty anxiety ya kununua magari kwa kujionesha.
 
Kweli Jamii Forums kwishney, mpaka imefikia kujadili huyu kibaka Godlove asie na mbele wala nyuma anaetumia ujinga wa wabongo kupiga pesa,. Great thinkers wamefikia this low???
 
Ukiona mtu anajitangaza mitandaoni kuwa yeye ni Tajiri mpotezee. Hii ni Kwa sababu utajiri haufichiki, kama mtu anao utajionesha Wenyewe bila kupigiwa promo.
 
Hii mitandao inalipa pesa nyingi kupitia content kama hizo, na yeye anaendelea kupiga hela kupitia watu kama nyinyi.

Akiona hivi anafurahi anajua mnamfuatilia.
 
Ya Chief au ya Bingwa?
Ya chief, ya huyo jamaa sio maybach, wameivalisha madubwasha ya maybach mkuu 😁😁 ( kwa ufupi ya chief sio wala ya huyu sio ) ni sawa na raia kuvaa gwanda za jeshi hazifanyi awe mwanajeshi ila anakuwa na muonekano wa kijeshi
 
Ya chief, ya huyo jamaa sio maybach, wameivalisha madubwasha ya maybach mkuu 😁😁 ( kwa ufupi ya chief sio wala ya huyu sio ) ni sawa na raia kuvaa gwanda za jeshi hazifanyi awe mwanajeshi ila anakuwa na muonekano wa kijeshi
Maybach mlango wa nyuma unafunguka na kioo chake?
 
Back
Top Bottom