Pambaneni na maisha yenu vijana, achaneni na mambo ya wengine.
Mkuu,
Kwenye saikolojia kuna anxieties nyingi sana. Kuna status anxiety, kuna poverty anxiety.
Kuna watu wamekulia kwenye umasikini kupata gari kwao ni ndoto.
Wakati mimi nilipokuwa na miaka 14 nilisoma kwenye kitabu cha baba yangu kinaitwa "Swim With The Sharks Without Being Eaten Alive : Outsell, Outmanage, Outmotivate, and Outnegotiate Your Competition" cha Harvey B. Mackay.
Kitabu kina mambo mengi sana, yameandkwa kifupifupi na kirahisi kusoma, hata mimi nikaweza kupata vitu.
Kitu kimoja alichoandika ni kwamba, nunua nyumba za bei kubwa na magari ya bei ndogo. Kwa sababu magari yanashuka thamani na real estate inapanda thamani.
Sasa kama ushaondoa ulimbukeni wa kupanda mabenzi na ma Range Rovr tangu utotoni, hata ukinunua ukubwani unanunua kwa kupata usafiri wenye standrd fulani tu, si kwa poverty anxiety na status anxiety ya kujionesha kwa watu.
Wabongo wengi wapo katika status anxiety na poverty anxiety ya kununua magari kwa kujionesha.