Chief Godlove: Nimepewa onyo la mwisho video niliyolia nikitoa siri

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mfanyabiashara Godlove Mwakibete, maarufu kama Chief Godlove, ameeleza kuwa maisha yake yapo hatarini baada ya kuitwa nchini Nigeria na kupewa onyo la mwisho kufuatia hatua yake ya kutoa siri za mtandao wa kishetani aliodai kujiunga nao hapo awali.

Akifunguka hivi karibuni, Chief Godlove amebainisha kuwa msukosuko huo unatokana na video aliyorekodi hivi karibuni mubashara kupitia mtandao wa TikTok Live, ambapo alionekana akilia kwa majuto na kukiri kufanya makosa makubwa ya kuingia kwenye kundi hilo kwa tamaa za fedha na utajiri wa haraka.

Akieleza chanzo cha maamuzi hayo, Mwakibete ameweka wazi kuwa alikumbana na maisha magumu na umaskini uliopitiliza wakati anakua chini ya malezi ya baba yake ambaye ni mchungaji maisha yaliyotawaliwa na shida za kukosa mahitaji ya msingi kama vile kuazima mboga kwa majirani na nyakati zingine kula ugali kwa chumvi.

Ugumu huo wa maisha ulimfanya ajenge tamaa kubwa ya kusaka mafanikio kwa njia yoyote ile, hali iliyomfikisha kwenye mtandao huo wa siri. Hata hivyo, kutokana na tishio na msukosuko mkubwa anaokabiliana nao sasa hivi kutoka kwa viongozi wa kundi hilo nchini Nigeria, Chief Godlove ametoa wito kwa umma na wanahabari kusitisha mara moja kumhoji au kuendeleza mijadala kuhusu suala hilo ili kulinda usalama na maisha yake.
1790316368114.png
 
View attachment 3677366
Huo mtandao tupeni namba zao
 
Huo mtandao tupeni namba zao
Na wewe unaamini kuwa ni kweli ana huo mtandao?ukienda kichwakichwa utaambiwa changia laki 1 ili upewe siri mwisho wa siku akipata watu 10 kwa siku anaishi vizuri mjini na kukodi magari kisha watu wanaamini kweli hela zake zimetokea freemason kumbe ni hela hizohizo mnazomchangia nyinyi
 
Matapeli wakiishiwa mbinu na kuanza kuporomoka huanza kutafuta visababu mapema vya kujihami
 
Na wewe unaamini kuwa ni kweli ana huo mtandao?ukienda kichwakichwa utaambiwa changia laki 1 ili upewe siri mwisho wa siku akipata watu 10 kwa siku anaishi vizuri mjini na kukodi magari kisha watu wanaamini kweli hela zake zimetokea freemason kumbe ni hela hizohizo mnazomchangia nyinyi
Hahaha ndio maana nine wachallenge kama huo mtandao upo watupe connectiona😅
 
Na wewe unaamini kuwa ni kweli ana huo mtandao?ukienda kichwakichwa utaambiwa changia laki 1 ili upewe siri mwisho wa siku akipata watu 10 kwa siku anaishi vizuri mjini na kukodi magari kisha watu wanaamini kweli hela zake zimetokea freemason kumbe ni hela hizohizo mnazomchangia nyinyi
Huu utapeli gani unaofanyika kwa kiasi kubwa hivi mpaka mtu kumiliki Mali za mabilioni HALAFU hakamatwi Mimi naamini haya mambo ya Hela za manyoka yapo
 
Hapana mkuu.
Matapeli wana mtandao mpana kama unavyoona wauza madawa ya kulevya.
Ukijaribu kumchimba sana au kumkomalia umpeleke mahakamani unapotezwa na matapeli wakubwa waliojificha nyuma yake.
Na hizo gari na nyumba anazotumia sio za kwake kunakuwa na wadhamini nyuma yake ambao wakipiga matukio wanagawana asilimia
 
Huyo kaishiwa sasa anatafuta sababu au mlango wa kutokea, hapo anawaleta ili hata akienda kufungua kanisa awe na legal reason ya kufanya hivyo, tena akifungua kanisa ndio atapiga pesa nyingi coz tayari ashaiweka hadhira katika plot nzuri Sana ya mkondo huo...Kuna wajinga walimuamini Sana na kuambatana naye, katika maisha Lazima uwe na makini na watu wa kuambatana nao mitandaoni.
 
Hii ni kututoa mchezoni tusishughulike na mambo ya siasa!! FREE LISSU.
 
Back
Top Bottom