kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kitu cha kwanza walichokifanya wakoloni walipokuja kwetu ni kutuambia kuwa kila kitu chetu hakifai, ni duni, ni uchenzi. Hii ikasababisha watu wabadilishe hata namna ya kuvaa, kuchana nywele, kula, matibabu, ulinzi na utawala. Tulifuta kabisa tawala na viongozi wa jadi na kukumbatia utamaduni wa kimagharibu ambao ni ngumu kuuzoea na kuufuata wote kama walivyo wao. matokeo yake serikali zetu ni za kimagharibi lakini watu wake wengi ni wa kijadi na kiasili. Serikali inajifanya haina dini, haina mila lakini watu wake wana dini zao, mila zao. Hakuna taifa lolote lile duniani ambalo halina dini na mila zinazofanana na dini na mila za watu wake lililofanikiwa hapa duniani.
China, Marekani,Uingereza, Saudi Arabia, Dubai, Urusi, Ugerumani, nk mataifa yao dini zao maalum ingawa kuna watu wa dini tofauti. Kwani tuone ajabu Rais Samia kuitwa chifu na kutumia machifu wa makabila yetu kutatua baadhi ya mambo yanayoihusu jamii husika? Kwanini tuwe na serikali isiyotambua machifu, dini za jadi, matibabu ya jadi, njia za jadi na uchawi katika kuihudumia jamii? Kazi yetu ni kukamata machifu, waganga wa jadi, watengeneza silaza za jadi, bunduki za jadi na wachawi badala ya kuwatambua, kuwakusanya, kuwaendeleza na kuwatumia katika kutatua kero mbalimbali za nchi kama vile mimba za utotoni, wizi wa mali ya umma, na ulinzi wa taifa? Mfano, kama kuna mchawi ambae anaweza kufanya uchawi ambao mwanaume akimtongoza mwanafunzi awashwe na kujikuna mwili mzima kwanini asiruhusiwe kufanya hiyo dawa?
Mfano, Tanzania tunaweza kutumia mila na desturi zetu katika kuzuia wizi pale TRA, madini, benki na kwenye mashirika ya umma. Kama kuna watu (waganga wa jadi) wanaoweza kusababisha mwizi ashindwe kuondoka na kitu alichokiiba kwanini sayansi hiyo isitumike kulinda fedha zetu pale TRA na mashirika yetu ya umma? Yaani na sisi tunaona kuwa sayansi hiyo ni ya kishenzi? Kama kuna mtu anaweza kusababisha
Wachina na wengine wanatumia mila zao kwenini sisi tusitumie mila zetu na kuna wengine wanamuona chief hangaya hastahili kukutana na machifu. Kukumbatia mila za watu wengine ndio chanzo cha shida zetu za ushoga, wizi wa kalamu, vitambi, nk