Chief Karumuna mgombea ubunge (CHADEMA) Bukoba mjini afunguka alivyotekwa 2020

Chief Karumuna mgombea ubunge (CHADEMA) Bukoba mjini afunguka alivyotekwa 2020

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
25 February 2023
Bukoba, Tanzania

MKUTANO WA HADHARA WA CHADEMA TOKA KIWANJA CHA MAYUNGA BUKOBA


Mbunge wa roho za watu katika jimbo la mioyo ya wakazi wa Bukoba mjini afunguka alivyotekwa na wenye bunduki 4 kwenye uchaguzi wa 2020.

Hayo yalijiri wakati CHADEMA walivyofungua mkutano wa hadhara na kusisitiza katiba mpya ili nchi iende vizuri.


Chief Karumuna amezungumzia kwa kina alivyotekwa na watu wenye bunduki 4 mara baada ya uchaguzi wa Oktoba 2020 na kukosa fursa ya kwenda kuhesabu kura ktk ofisi ya Halmashauri na baada ya hapo kupewa kesi hatari sana.

Leo jeshi la polisi tarehe 25 February 2023 wametekeleza jukumu lao vizuri kusimamia usalama wa raia tofauti na miaka 7 iliyopita.

Kuhusu maendeleo ya Bukoba mjini, wafadhili walipiga saluti walipokuta utawala bora mjini Bukoba uliokuwa chini ya CHADEMA lenye baraza la madiwani la mchanganyiko wa madiwani toka CHADEMA, CUF na CCM kabla ya uchafuzi wa uchaguzi wa 2020

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA mkoa wa,Kagera akiwemo wakili Dustan Mutagahywa katibu wa CHADEMA mkoa wa Kagera akazungumzia kero mbalimbali zinazohitaji ufumbuzi
 
Watu wameteswa sana wengine hawana majukwaa ya kusemea.

Itoshe kusamehe na kuendelea na maisha kama ambavyo Meya mstaafu ameshauri.

Mungu anayashuhudia na kuyashughulikia.
 
Anachofanya Chadema, nikuwaambia wananchi kwamba Rais Magufuli alikuwa kiongozi mbaya sana, ila Rais Samia ni kiongozi mzuri sana! Hivyo Samia (CCM) anapigiwa campaign.!
 
Back
Top Bottom