Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..

Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kwa wale wenzangu na miye watavikumbuka vizuri "Mfululizo" wa vitabu vya "Ujinga wa Mwafrika". Vitabu hivi vilikuwa kwa muda mrefu sehemu ya simulizi la "Mazungumzo Baada ya Habari" na vilisimulia hadithi fulani ya maisha wakati wa ukoloni au baada ya ukoloni na jinsi gani Waafrika tulikuwa hatujui vitu vya wageni na hivyo tulijikuta tunafanya vitu ambavyo baadaye tukivifikiria tunacheka.

Lakini mojawapo ya vitu ambavyo vinatokana na somo hilo ni habari ya jinsi gani mababu zetu walivyoweza kuuza utajiri wa ardhi yao kwa wafanyabishara ya ukoloni ambao kinara wao alikuwa Carl Peters (Mkono wa Damu)- Mjerumani. Sasa Carl Peters ndiye kwa kiasi kikubwa alisababisha Ujerumani itafute makoloni Afrika na alifanya hivyo baada ya kuona Waingereza na Wabelgiji (Chini ya Mfalme Leopold II) wakitanua maeneo ya mamlaka yao.

Carl Peters alipokuja maeneo haya ya Tanganyika enzi hizo alijileta kama Mwakilishi wa Ujerumani na akabuni mikataba mbalimbali ambayo aliingia na machifu na watawala mbaalimbali (akiwemo Sultani wa Zanzibar na Kabaka Mwanga wa Uganda) na alifanya mikataba hiyo kwa niaba ya kampuni aliyoiunda ya German East African Company (mliosoma historia mtaikumbuka).

Mojawapo ya mikataba hiyo ule maarufu wa Chifu Mangungo wa Usagara na mingine mingi. Katika mikataba yote hiyo machifu walikuwa wanakubali kuyaachilia maeneo ya ardhi yao kuwa chini ya ulinzi wa Mjerumani na kutumiwa kwa faida ya Mjerumani kwa milele yote. Wengi tunafahamu kuwa wazee hawa walikubali kwa sababu moja kubwa walikuwa hawajui kilichomo kwenye mikataba hiyo na hivyo hata walipokuja kugundua kuwa wameuza ardi yao "mikataba" ile ilikuwa halali na Ujerumani ilikuwa tayari kuhakikisha inasimama hata kwa vita (Kilimanjaro ni mfano mmoja wapo).

Mikataba hii ilifichwa kwa wenyewe na ilifanywa na watawala wao; wakulima na wanakijiji wengine hawakujua kuwa machifu wao wameuza ardhi yao. Na hata kama wangetaka kujua wasingeweza kujua kwani mikataba ilikuwa ni siri kati ya watawala na kampuni hiyo ya kigeni. Na hivyo ndivyo kihistoria eneo ambalo baadaye lilikuja kujulikana kama Tanganyika lilivyoangukia mikononi mwa Ujerumani - hii ilijumuisha Rwanda na Burundi. Hii ilibadilika baada ya vita ya kwanza ya dunia ambapo Tanganyika ikawekwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa kupitia Uingereza.

Mjerumani kwa kutumia kampuni ya GEAC kujenga reli, kuanzisha mashamba ya katani, pamba n.k na vyote hivi vilifanywa si kwa ajili ya kuwanufaisha wazawa au wananchi bali hatima yake mazao yanayopatikana yapelekwe Ujerumani kuwa malighafi katika viwanda vyao na zile nyingine za kuuzwa sehemu nyingine kuwa chanzo cha mapato kwa Ujerumani. Wananchi hawakuwa na uchaguzi wowote wa nini kinapandwa, nani anasimamia na hata hawakuwa na uamuzi juu ya matumizi ya faida ambayo Mjerumani alikuwa anapata. Hapa ndipo ulipokuwa Ujinga wa Mwafrika.

Sasa ujinga si ugonjwa au tusi; ujinga ni hali ya kutokujua (ignorance). Mtu aliye mjinga akijuzwa anaerevuka na ujinga humtoka katika lile jambo ambalo alikuwa halijui. Na kila mwanadamu ana ujinga wa aina fulani na hivyo katika maisha yote anatakiwa awe tayari kujifunza. Lakini kwenye eneo ambalo ufahamu upo tayari na unapatikana mtu hatakiwi kuendelea kuwa mjinga. Ujinga wa aina hiyo ambao mtu anauchagua ndio huitwa upumbavu au wengine wanaitwa ujuha kwani ni mtu ambaye hata akijuzwa hajui na hawezi kujua kwa sababu hayuko tayari kujua!

Leo hii watawala wetu wametuambia mikataba ni siri na kuwa mikataba hiyo ikiwekwa wazi basi wawekezaji wanaweza kukimbia na kuwa mikataba hiyo ni siri kati ya 'serikali na wawekezaji' hata kama inahusu ardhi ya umma na mali umma. Ujinga ni kuwa tumekubali kuwa hilo ni kweli! Na ujinga zaidi ni kuwa watawala wetu wanaingia mikataba na wanaamini ni vizuri kuifanya siri na hivyo hatujui nini kilichomo. Mkataba ule wa Carl Peters na Chief Mangungo ulikuwa na kipengele kinachosema kuwa ardhi hiyo ingeweza kutumiwa "exclusively" kwa matumizi ya Mjerumani.

Kwanini nimesema hili....

Well, mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi kati ya Kampuni ya Kichina na serikali (Chief Mangugu wa leo) una kipengele kinachosema kuwa sehemu ya gesi ambayo itakuwa inachimbwa huko itauzwa kwa China. Hivyo Wachina wamehakikishiwa gesi ya Mtwara na kutokana na ujuzi wa mtu aliyenisimulia hili na ameona mkatbaa huo anasema Wachina wamehakikishiwa kwa asilimia...

Na sisi tumekubali, Wabunge wamekubali

Mikataba siri....

Ujinga wa Mwafrika 2.0
 
Ndio maana linapokuja suala la ku-expose mkataba/mikataba watu wanakuwa mbogo.
 
Swali linaweza kuulizwa: ni nani aliye mjinga baina yetu? Wao wanaotuambia kuwa mikataba iliyosainiwa ni siri yao tuwaamini au sisi tunaokubali kuwa ni siri tukiamini walichotuambia?

Labda na mimi niuulize swali, tuseme mikataba yote iwekwe wazi, ni nini kitabadilika? hata kama ikijulikana Gesi yote kapewa Mchina au mwingine yoyote ni nini kitabadilika? Ni mangapi sasa tunayajua na yako wazi ni nini kimefanyika? Kuna fungu kubwa la kupeleka viongozi wote wa Serikali na Chama (pamoja na Upinzani) kwenda kutibiwa nje ya nchi pindi wauguapo kila mtu anajua hilo, kuna lolote linafanyika? Mbona tuko kimya? kuna usaliti mkubwa zaidi ya huo ukichukulia watu wanakufa wodini kwa kukosa tu dawa?

Wakati wa ukoloni vibarua waliokuwa wanafanya kwenye mashamba ya katani Tanga na kwingeneko ujira waliokuwa wanalipwa ingawaje ulikuwa mdogo lakini uliwatosha kula mpaka pale ujira mwingine ulipofika, leo hii kibarua pesa anayopata haitoshi hata wiki moja, na kusema kwamba mazao yaliwanufanisha wao (Wajerumani) tu sio kweli kwa maana Wakulima wa Kilimanjaro (Waafrika) tayari walikuwa wanashindana na wakulima wa Kijerumani kwa Uzalishaji wa Kahawa, leo wamerudi nyuma miaka 100!

Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukaa na kujitafakari sisi kama Watz, tatizo letu ni nini na liko wapi, turudi nyuma tuangalie tulipokosea, kuanza kukaa na kulaumu na kutafuta visingizio hakutatusaidia kitu, tujiulize ni kwa nini tunashindwa kusimamamia maslahi yetu?

Usiri wa Mikataba sio tatizo, utakuta kuna nchi nyingi pia Mikataba ni siri lakini cha muhimu wale wanaosaini hiyo Mikataba HAWAWEZI kukubali kuikandamiza nchi yao kama sisi tunavyofanya, sasa swali ni KWA NINI?

Ukiangalia hivi majuzi Raisi Kikwete alikuwa Ufaransa kuna picha wamepiga na Raisi wa Ufaransa na watu wake kwenye meza, nina uhakika kuna Mkataba umesainiwa pale na siajabu pia watu wa Ufaransa hawaujui lakini nina uhakika wale waliousaini kwa upande wa Ufaransa maslahi ya nchi yalizingatiwa kwanza, lakini sisi kwetu Mungu ndio anajua, sasa kwa nini?Tutafute jibu hapo, yani ni kwa nini mtu awe tayari kuweka nchi yake na watu wake rehani kwa miaka 99? Bila kupata hilo jibu hatuwezi kutatua hili tatizo tutabaki tu kufikiri tatizo ni CCM, tutaitoa na baada ya muda tutarudi hapahapa tena kuanza kujadili yale yale wakati huo adui hatakuwa CCM tena!
 
Kwa nini mikataba ya mambo ya umma iwe ya siri?
 
Ujinga wetu ni kuendelea kuchaguwa CCM itawale.

Kwani waafrika wote wapo CCM hapa unaelezewa ujinga wa Mwafrika siyo ujinga wa Watanzania kama unavyotaka.
 
Kwanini nimesema hili....

Well, mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi kati ya Kampuni ya Kichina na serikali (Chief Mangugu wa leo) una kipengele kinachosema kuwa sehemu ya gesi ambayo itakuwa inachimbwa huko itauzwa kwa China. Hivyo Wachina wamehakikishiwa gesi ya Mtwara na kutokana na ujuzi wa mtu aliyenisimulia hili na ameona mkatbaa huo anasema Wachina wamehakikishiwa kwa asilimia...

Na sisi tumekubali, Wabunge wamekubali

Mikataba siri....

Ujinga wa Mwafrika 2.0

Mkuu wangu hapo kwenye rangi sina tatizo na hilo ikiwa bei ya kuwauzia itaamuliwa na soko (hakuna fixed price) na pia pasiwe na kipengele cha kutupangia kiasi cha kuuza nje ya soko lao bila kusahau kusiwe na masharti ya upande wao TU pale tutapokiuka masharti ya kuwauzia wao na sio pale kutapokuwa na any default kutoka kwao inayoweza kutishia mauzo ya gesi yetu nje ya wao.
 
Swali linaweza kuulizwa: ni nani aliye mjinga baina yetu? Wao wanaotuambia kuwa mikataba iliyosainiwa ni siri yao tuwaamini au sisi tunaokubali kuwa ni siri tukiamini walichotuambia?


Cha kujiuliza kwanini wawekezaji wanaamini "siri" zao zitatunzwa vyema na wao (akina Chief Mangungo) tu?
 
Ujinga wa mwafrika unaendelea.
Hata mkataba halisi wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar umefanywa kuwa ni siri. Hakuna mtu,taasisi au serikali ambayo inakiri kuwa mkataba huo upo na kuuonesha kwa waafrika wajinga!

Kwa Tanganyika hili ni ujinga wa mwafrika 2.0

Mikataba ya migodi ya dhahabu, Richmond/Dowans, ATC na Allience, Rada na ndege ya Rais ni ujinga wa mwafrika 3.0

Haya ya mikataba ya gesi na bomba itakuwa ni ujinga wa mwafrika 4.0 au 5.0 kwenda mbele.

Tatizo letu ni kuwa bado tunaamini katika mazingambwe/viini macho na bendera kufata upepo.
 
Excellent article.
Make sure it gets posted by Daily Paper News etc over & over again so that it makes headlines.
JK needs to be embarassed until he runs back to his cave.
They really take advantage of ignorant naive africans.
 
Right MTAZAMO,
Kuuzwa kwa GAS kwa China Si tatizo endapo itakuwa bihashara kama nyingine lakini zenye maslahi kwa taifa na watu wake. Kikubwa ni mkataba uwe wazi ili tusije kuingia katika mikataba feki Kama mingine iliyo na inayozidi kupoteza rasilimali za taifa bila ya kuwa na faida halisi kwa mtanzania.
Kwa Gas tuliyonayo na matumizi yetu Kama nchi hasa za ukanda wetu wa equator ambazo matumizi ni madogo ukilinganisha na nchi za baridi tunastahili kufanya bihashara katika katika hili ila kwa umakini wa bei manufaa kwa watanzania kwa ujumla. China anaweza kupewa priority lakini kwa kwendana na soko kulingana ubora.
 
mikataba ihusuyo raslimali zetu wote lazima tuione wote. hizo raslimal si mali ya rais, wazir wala yeyote yule. ni zetu wote. kuficha mikataba kama hii ni hatari kwa ustawi na usalama wa taifa.
 
Wawekezaji wanasema ukilazimisha iwekwe wazi wataacha kuwekeza nchini na sisi tutaendelea kuwa maskini....at least that what watawala wetu wanasema.

wanakuja kuwekeza kwasababu wanataka faida. kwahiyo lazma waje. wazungu, wachina. tatizo nionalo wawakilishi wetu kwenye mikataba wanataka cha juu na ushahid ni kule uswisi. kwa namna hiyo si mwekezaj atakayetaka kuficha mkataba bali mwakilshi wetu hasa. hataki kuonekana juha. anyway mwekezaj hatotaka aonekane mnyonya
 
Mzee Mwanakijiji

Freedom of Information Request should be a constitutional right which can be challanged in the court of Law. Secondly I'm not in favour on all contracts to be made on public but I'm in favour of allowing the Member of Parliamnet and especially the Leader of the oppostion in the parliamnet to have access to all contracts exceeding usd 100,000 and this should be part of the law of the land.

Doing this will strike balance between transparency and secrecy.
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini mikataba ya mambo ya umma iwe ya siri?

Sizani kama ni lazima hata kuweka hii mikataba hadharani, Ila kuna ulazima ku safeguard kwa Kuhakikisha kwamba kiongozi wa Upinzani Bungeni anapata nakala zote za mikataba, then serekali kwa kushirikiana na Upinzani wanaweza kutengeneza talking point za mkataba ambazo zitakuwa verifibale.
 
Back
Top Bottom