Wapigania Uhuru walipigania maslai Yao binafsi kupitia mgongo wa waafrika wengi
Kweli kabisa tunaona jinsi vyama vya ukombozi wanasiasa wake walivyojigeuza wakoloni weusi na kujipendelea kwa kujirundikia mali, kupeana vyeo kwa kujuana na kibaya zaidi kushindwa kuendeleza uchumi na upatikanaji wa nishati kama ya umeme wa maji, makaa ya mawe, upepo, jua ili kuendeleza viwanda kupatikane ajira na kusindika mazao ya nafaka, matunda, mazao ya uvuvi na wanyama ili kuongeza thamani ya bidhaa na maendeleo ya watu.