Chifu Mwakatumbula wa Wanyakusa akabidhiwa Ikulu ya kichifu leo...Imejengwa mwaka 1900

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
2,659
Reaction score
2,827
IMG-20221001-WA0028.jpg
Katika kutekeleza adhima ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan ambaye ni kiongozi wa machifu nchini Chifu 'Hangaya' ya kuuhuisha kuendeleza tamaduni za kichifu nchini, Hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa ,Chifu Edwin Mwakatumbula leo amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.

Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1900.

Aidha amesema kuwa kazi aliyokabidhiwa na machifu wadogo wa kabila hilo ataendelea kuifanya kwa kuzingatia mila na desturi za kabila hilo maarufu nchini.
IMG-20221001-WA0030.jpg

Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanyakyusa wote nchini.

Chifu Edwin amesema kuwa ,jamii ya wanyakyusa nchini wanapaswa kujivunia hali ya amani na umoja miongoni mwao huku akihaidi kuendela kulilea kabila hilo kwa kuzingatia misingi na tamaduni zao.

Mbali ya kuwa Chifu, Edwin anahistoria kubwa kwenye siasa za nchi hii, huku akihudumu kwenye nafasi mbalimbali za kiungozi na kiutawala kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa nyakati tofauti amehudumu kama Katibu wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya ambapo mara ya mwisho alikuwa katibu wa chama wilaya ya Geita.

Chief Edwin ni miongoni mwa watoto 129 wa marehemu Chief Bentamanile Mwakatumbula wa kabila ilo ambaye alifariki dunia mwaka 1955 huku akicha wake 52 .

Vitabu vya kihistoria vya kabila la Wanyakyusa vinamtambua Chifu Bentamanile Mwakatumbula kwa mageuzi makubwa ya kiutawala aliyoyafanya wakati wa utawala wake wa miaka 45.

Katika kuthibitisha hilo, Alikuwa Chifu pekee kutoka Tanganyika aliyekabidhiwa Cheti cha heshima kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Wakati wa utawala wake, alihesabiwa miongoni mwa machifu wa kimila waliokuwa mstari wa mbele kuipambania nchi uhuru, huku Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius K Nyerere akisema kuwa kazi kubwa waliyoifanya kipindi hiko katika Mikoa ya kanda za juu kusini hususani mkoa wa Mbeya zilikuwa za kutukuka na kurahisisha kuiunganisha nchi.
 
"Uchifu Kwa dhana ya kutunza utamaduni wetu na kulinda mila zetu na kujulisha/kurithisha/kuelimisha kizazi hiki tulipotoka"
THANK YOU CHIEF HANGAYA.
 
Uchifu ungerudishwa uwe na hadhi kama chiefdom za Uganda. Sioni ubaya wa makabila kuwa na Machifu wao ili kuemdeleza mila na desturi zao
Hakuna la maana zaidi ya uchawi wangefuta kabisa
 
View attachment 2374003Katika kutekeleza adhima ya Mhe Rais Samia Suluh Hassan ambaye ni kiongozi wa machifu nchini Chifu 'Hangaya' ya kuuhuisha kuendeleza tamaduni za kichifu nchini, Hatimaye Chifu wa kabila la Wanyakyusa ,Chifu Edwin Mwakatumbula leo amekabidhiwa Ikulu yake ya Kichifu na kiongozi wa machifu wadogo wa kabila hilo.

Akizungumza katika tukio hilo la kihistoria, Chief Edwin amesema kuwa imekuwa siku ya baraka kwenye himaya hiyo, kwa yeye kukabidhiwa Ikulu hiyo iliyojengwa Mwaka 1900.

Aidha amesema kuwa kazi aliyokabidhiwa na machifu wadogo wa kabila hilo ataendelea kuifanya kwa kuzingatia mila na desturi za kabila hilo maarufu nchini.
View attachment 2374004
Amesema kuwa aliporithi uchifu wa kabila hilo kutoka kwa marehemu Chifu Daudi B Mwakatumbula miaka 10 iliyopita amejitahidi kuendeleza mila za kabila hizo huku akidumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wanyakyusa wote nchini.

Chifu Edwin amesema kuwa ,jamii ya wanyakyusa nchini wanapaswa kujivunia hali ya amani na umoja miongoni mwao huku akihaidi kuendela kulilea kabila hilo kwa kuzingatia misingi na tamaduni zao.

Mbali ya kuwa Chifu, Edwin anahistoria kubwa kwenye siasa za nchi hii, huku akihudumu kwenye nafasi mbalimbali za kiungozi na kiutawala kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa nyakati tofauti amehudumu kama Katibu wa Chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya ambapo mara ya mwisho alikuwa katibu wa chama wilaya ya Geita.

Chief Edwin ni miongoni mwa watoto 129 wa marehemu Chief Bentamanile Mwakatumbula wa kabila ilo ambaye alifariki dunia mwaka 1955 huku akicha wake 52 .

Vitabu vya kihistoria vya kabila la Wanyakyusa vinamtambua Chifu Bentamanile Mwakatumbula kwa mageuzi makubwa ya kiutawala aliyoyafanya wakati wa utawala wake wa miaka 45.

Katika kuthibitisha hilo, Alikuwa Chifu pekee kutoka Tanganyika aliyekabidhiwa Cheti cha heshima kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Wakati wa utawala wake, alihesabiwa miongoni mwa machifu wa kimila waliokuwa mstari wa mbele kuipambania nchi uhuru, huku Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius K Nyerere akisema kuwa kazi kubwa waliyoifanya kipindi hiko katika Mikoa ya kanda za juu kusini hususani mkoa wa Mbeya zilikuwa za kutukuka na kurahisisha kuiunganisha nchi.
machifu waupige mwing basi wafute tozo
 
Ikulu hii ya 1900??? Au ikulu ya 2020?? Kwa maana ya jengo??

Miaka kumi alikuwa ana ongoza bila ikulu?
 
Back
Top Bottom