Chikawe afichua siri: Vifungu 6 Katiba mpya vilichomekwa bungeni bila kuhusisha Zanzibar

Mkuu nimelisoma gazeti la Nipashe na nimesoma vizuri hata bandiko lako ambalo pengine sana sana ume amplify yaliyo andikwa na Nipashe.
Naamini vile vile wewe ni mtu wa ku reason na kuelewa logic.
Dhahma ya yaliyojiri Bungeni , CHADEMA na vyama vingine wanamrushia Ndugai, your weak point.
Lakini CHADEMA na vyama vingine havisemu kuwa VILISUSIA mchakato huo at their own peril!!!

Wapinzani ni wachache kuliko wa CCM-kwa hivyo ule msemo uitwao -"wewe susia, wenzio twala" umetumika hapo, mbaya zaidi wapinzani ambao ni wachache hawana effect yoyote wakisusia.
Kwa hiyo kimchakato Bungeni, wapinzani hawana chao, walisusa at their own peril.

Katika gazeti la leo la Raia Mwema , pengine Mzee Wassira ameliweka vizuri zaidi na kasema:

"Jambo la msingi ambalo nataka kusema hapa ni kwamba wapinzani walipotezahaki ya kuupinga huu mswaada mara baada ya kuamua kukimbia bungeni. Pale ndio mahala pekee ambako sheria zinatungwa.

Sheria hazitungwi Ikulu wala Jangwani. Sasa wao sehemu halali ya kutunga sheria wanazira halafu wanataka sheria zikatungwe na Rais Ikuluau na wananchi pale Jangwani, Haiwezekani..."


Kwa kifupi hapa ni dhahiri kuwa CHADEMA , CUF na wengine wameingizwa mjini na wanasiasa wanasheria uchwara kama Lissu, kwa kushauriwa kuwa wanaweza kupinga sheria nje ya mchakato wa Bunge.


Mengine wanasahau kirahisi, si suala la kodi ya simu tunaliona?
 
Huyu mbunge wa kisarawe alotoa Wazo hili hajitambui tume ya Warioba ukivunja maoni hayana msimamizi wa kuyatetea Warioba ataitwa km Mtu wa kawaida hatambuliki kisheria nguvu Hana ya kusimamia maoni kashang'olewa meno badala ya kusimamia matatizo ya kwao uzaramoni maji Hakuna barabara ya lami Hakuna ni km 75 kutoka dar umasikini wakitisha kisarawe mashamba wanauziwa wageni yeye analeta ukada bungeni wabunge Kama Hawa ni wakuchapa bakora kashashiba anaongea utumbo bungeni jiulize jafo dar ilikuwa ya wazaramo Leo Nipo?na tutawafuata hukohuko chole kununua mashamba yenu.
 
una copy habari ndefu then una post mara tatu, acha uhuni

Hebu tuambie,nani mhuni.Ni Chikawe na wenzake wanaoongea kila mmoja na lake kana kwamba hawajui wanachokisemea au ni mleta uzi aliye-"copy" na ku-"paste" mara tatu.Inaonyesha jinsi mleta mada alivyo na uchungu na mambo yalivyoendelea bungeni.Hakuna boya tena leo hii wa kukubali kila kitu.Amka ndugu,tena amka leo maana upepo wa mabadiliko hakuna awezae kuuzuia,na ukijidanganya ukaamka kesho utakuta umechelewa na Chikawe na wapambe wake hawatakusaidia lolote,ni sisi wanyonge ndo tunaosaidiana
 

Bado sijaona tatizo lako maana kama umesomahabari hiyo gazetini ni kifungu gani katika habari hiyo nimekiongeza? Nilichofanya ni kuchangia mada kama we ufanyavyo wakati mada hiyo ilivyo imechukuliwa kama ilivyo toka gazetini bila hata uhariri wa kuunganisha paragraph nisijepoteza utamu wa habari hiyo.

Kwa taarifa yako upitishwaji wa mswada huo bungeni licha ya malalamiko mengine, kuna kosa moja ambalo huenda kikao kijacho cha bunge likapekuliwa bungeni kwa kupitisha mswada huo kinyume cha sheria kwa idadi halali ya wajumbe wa bunge bungeni. Wabunge waliopitisha mswada huo walikuwa punguvu ya theluthi moja ya wabunge wote, hilo tu ni kasoro tosha moja wapo.

Kwa mtazamo huo Ndugai hana upeo wa sheria bungeni pamoja na wabunge wa CCM vinginevyo wangeweza kubaini hilo kabla ya kuamua kupitisha ajenda hiyo. Mara kadhaa vikao vya nyuma wabunge wa upinzani wamekumbushia kiti cha speaker kutaka kupigia kura mswada wakati wabunge wako pungufu ya idadi kisheria, inaonekana wazi wabunge wa CCM ni bora liende bungeni.
 
Ndiyo maana wananchi wana imani na Upinzani - sasa wangejuaje haya mambo kama wasingekuwepo kina Lissu. Na huu mtindo wa kuchomekea vifungu sasa umeanza kuota mizizi, hii mara ya pili sasa!!
 

Yule mwanamama Pindi Chana mbunge wa kuteuliwa mkoa wa mpya wa Njombe (Ludewa) anayeongoza kamati ya katiba na sheria bungeni ndiye mpishi na pengine mkolezaji viungo katika kuchomekea hivyo vifungu kienyeji kwenye kamati yake. Labda anataka kutengeneza mazingira ya kukubalika zaidi chamani maana inaelekea uwezo wake wa kupambana jukwaani kugombea ubunge jimbo la Ludewa hawezi kufurukuta mbele ya Jabali Filikunjombe wakati mswada wa katiba mpya hautoi matumanini ya kuendekeza upendeleo wa ubunge wa kupeana kishikaji.
 
Chikawe angalia mawazo ya watanzania usitunyime haki yetu shauri kwa maslahi ya watz sio ccm ili tuje tukukumbuke tatizo maslahi yenu ccm mumeweka mbele
 

Mkuu ndio maana nasema umeingia mkenge wa gazeti la Nipashe , kwa vile logically niliamini kuwa unaweza kuchanganua makosa ya gazeti hilo.
Kama ni kweli idadi ya waliopitisha muswaada huo ni pungufu ya two thirds inayotakiwa kikatiba , hilo laweza kuwa issue, lakini vinginevyo mseme bora liende au vyovyote vile , wapinzani ni the weak minority Bungeni, na ni vizuri wakalitambua hilo.
Hakuna kelele za chura zitakazo badilisha ukweli huo.
 

"Kazi ya wabunge kutoka Zanzibar ni kuwakilisha maslahi ya Wazanzibari ndani ya Bunge, kwa hiyo pamoja na kwamba vifungu hivyo havikupelekwa Zanzibar siyo tatizo, wawakilishi wao ambao ni wabunge walikuwapo, na huo ndio utaratibu wa kupitisha/kutunga sheria," alisema.

Huo ndo upimbi...vifungu vingine vimepelekwa Znz, vingine ambavyo havikupelekwa basi wabunge wanatosha kuwawakilisha wazanzibar.....hapa kuna tatizo!!! Kwanini havikupelekwa vyote au kwa nini basi wabunge wa zanzibar wasingewawakilisha wazanzibar kwa vifungu VYOTE????
 
Hilo swali waulize ndugu zenu CUF ambao leo mko pamoja pengine waulizeni vile vile wanapanda boti na mabasi kwenda Dodoma kula posho tu, na si kutumia akili zao kuwawakilisha wale watu wachache sana wanaowawakilisha katika Bunge la muungano?
Kwa kifupi sasa ndio mnatambua kuwa kususa kwenu ndo furaha ya walio wengi Bungeni, lakini kama wawakilish wa wananchi wsliowatuma wabunge wa vyama vya upinzani wamevurunda.
 

...kiukweli kwa mwanasiasa kuonyesha unweza mbele ya jamii ni kawaida,ila huyu mama anakosea sana,i strongly believe ana agenda ya siri aliyotumwa kuhakikisha inafanikiwa maana hana uwezo wa kubuni hivo vifungu na technique kama hizi dakika za mwisho za mswada, ametumwa na mpango uliratibiwa vyema na matokeo yake mpaka ndugai analazimisha mambo. Na naamini makinda aliwekwa kando maksudi ili kupisha songombingo hili. Tatizo kubwa la wabunge wa ccm ni kunyemelea uwaziri, wanajipendekezaa mpaka wanageuka misukule, they dont reason anymore na wengine wanatumwa tu...
 
 
 
Hii ni article kutoka kwenye media zingine au ni habari uliyoandika wewe mwenyewe?.

Kama umevuta kutoka kwenye media nyingine, weka SOURCE yake ili wachangiaji wapate mwanga wa kile wanachochangia kilipotoka, kuacha kuweka SOURCE wakati umevuta kutoka sehemu nyingine utaangukia kwenye kundi la watu wanaoingizwa kwenye kundi la wezi wa maandishi (Plagiarizer) na ambao wanataka sifa na pongezi ambazo hawastahili.

Wape wachangiaji haki wanayostahili kimaandishi nje ya hivyo utakuwa ni utapeli wa maandishi and cynicism.
 
Tushawachoka MAGAMBA hao dawa yao ni kuwapiga chini 2015,maana kila kitu wao wamezoea kuhodhi aaaah wanafikiri watatawala milele.
 
Nini usichoelewa, habari hiyo ambayo imekuwa published gazetini? Hujaelewa siri iliyotolea na Waziri Chikawe mambo ambayo yamelalamikiwa na vyama vya upinzani hali kadhalika tume ya katiba?

Huu ni uhuni uliofanyika bungeni ndio huuelewi?
Watu wengine uwezo wao wa kuelewa ni mdogO, wanategemea ZIDUMU FIKRA ZA MWENYE KITI
 

Unategemea nini kutoka kwa KITU MAALUM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…