Chikawe kuanza na kero ya rushwa polisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe.



WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe amesema atashughulikia tatizo la polisi kulalamikiwa kula rushwa kwa

kuwaandalia mazingira mazuri, ambayo hata akiulizwa kwa nini anakula rushwa hatakuwa na jibu.
Chikawe alisema hayo jana,wakati

akiripoti katika ofisi mpya kama Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kuteuliwa hivi karibuni, akitoka Wizara ya Katiba na Sheria.
Akiwa

wizarani hapo alipokewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo , Mbarak Abdulwakil na Naibu Waziri Pereira Ame Silima na wafanyakazi

wengine wizarani hapo. Alisema haipaswi kuwa na polisi asiyelipwa mshahara vizuri .
“Kabla hujaanza kulaumu polisi au mtu yeyote kwa

nini anapokea rushwa, ni vema kumtengenezea hali ambayo hata akiulizwa kwa nini anafanya hivyo atakosa jibu.
Lakini siyo kama

natetea vitendo hivyo, lakini ni vema kujiuliza kwa nini anafanya hivyo” alisema. Chikawe aliahidi kupambana na rushwa kadri awezavyo.

Alisema kutokana na wizara hiyo kuwa kubwa, siyo rahisi kufahamu kila linaloendelea.
Alisema atatoa namba maalumu ya Waziri,

kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na wafanyakazi walio chini ya wizara yake. Alisema anafahamu wizara ina changamoto

nyingi.
Alisisitiza atafanya kazi kwa kushirikiana na watumishi wote. Pia alisema atajifunza kutoka kwa Katibu Mkuu na Naibu Waziri,

ambao ni wazoefu katika wizara hiyo.http://www.touch.habarileo.co.tz/in...20983-chikawe-kuanza-na-kero-ya-rushwa-polisi
 

Attachments

  • chikawe.jpg
    8.3 KB · Views: 156
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…