Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe amesema atashughulikia tatizo la polisi kulalamikiwa kula rushwa kwa
kuwaandalia mazingira mazuri, ambayo hata akiulizwa kwa nini anakula rushwa hatakuwa na jibu.Chikawe alisema hayo jana,wakati
akiripoti katika ofisi mpya kama Waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kuteuliwa hivi karibuni, akitoka Wizara ya Katiba na Sheria.Akiwa
wizarani hapo alipokewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo , Mbarak Abdulwakil na Naibu Waziri Pereira Ame Silima na wafanyakazi
wengine wizarani hapo. Alisema haipaswi kuwa na polisi asiyelipwa mshahara vizuri .Kabla hujaanza kulaumu polisi au mtu yeyote kwa
nini anapokea rushwa, ni vema kumtengenezea hali ambayo hata akiulizwa kwa nini anafanya hivyo atakosa jibu.Lakini siyo kama
natetea vitendo hivyo, lakini ni vema kujiuliza kwa nini anafanya hivyo alisema. Chikawe aliahidi kupambana na rushwa kadri awezavyo.
Alisema kutokana na wizara hiyo kuwa kubwa, siyo rahisi kufahamu kila linaloendelea.Alisema atatoa namba maalumu ya Waziri,
kuwasiliana moja kwa moja na wananchi na wafanyakazi walio chini ya wizara yake. Alisema anafahamu wizara ina changamoto
nyingi.Alisisitiza atafanya kazi kwa kushirikiana na watumishi wote. Pia alisema atajifunza kutoka kwa Katibu Mkuu na Naibu Waziri,
ambao ni wazoefu katika wizara hiyo.http://www.touch.habarileo.co.tz/in...20983-chikawe-kuanza-na-kero-ya-rushwa-polisi