Chikulupi Kasaka Achukua Fomu ya Kugomea Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

Chikulupi Kasaka Achukua Fomu ya Kugomea Ubunge, Bunge la Afrika Mashariki (EALA)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Chikulupi Njelu Kasaka ambaye ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) tarehe 14.08.2024.

Chikulupi Njelu Kasaka amechukua fomu katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi iliyopo jijini Dodoma akisindikizwa na makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi

Chikulupi Njelu Kasaka ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na Wakili, ni mbobezi wa masuala ya siasa, utawala na diplomasia mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka12 katika mahusiano ya kimataifa na diplomasia.

Aidha, Chikulupi Njelu Kasaka amekitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nyanja tofauti na pia ni mjumbe katika kamati mbalimbali.

Baada ya kuchukua fomu hiyo, Chikulupi Kasaka akiongea na waandishi wa habari ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika kukuza umoja na uchumi katika jumuia ya Afrika mashariki.

Chikulupi Njelu Kasaka ameahidi kuiendeleza kazi hiyo ili kuiwezesha nchi yetu kupiga hatua kiuchumi kwa kuimarisha uchumi na fursa kwa vijana na taifa kwa ujumla

WhatsApp Image 2024-08-14 at 14.10.17.jpeg
WhatsApp Image 2024-08-14 at 14.10.18.jpeg
 
Back
Top Bottom