...Inawezekana pia sio mapenzi kwa maana ya mapenzi, bali ni ile Guilty conscious mtoto anayobakia nayo na kukua nayo.
Katika maisha yangu yote sijapata kumsimulia mtu yeyote yaliyonikumba utotoni. kwanza, kitendo kile nilijua wazazi wakijua ni bakora kwa kwenda mbele...
Pili, nilijua iwapo yule dada ataathirika kwa lolote mimi ndiye mkosa sababu nilimkojolea mkojo! Vile vile kwa wakati ule nilimuonea huruma huenda angetimuliwa kazi, au kuadhibiwa vibaya mno... hivyo kunifanya nimbebee mzigo wake wa dhambi!
Tatu, Japokuwa kitendo hicho kilinitokea nikiwa na miaka mitano tu, bado nakikumbuka mpaka leo (kwa woga ule) na kuna wakati natamani kumhadithia mzazi wangu kilichotokea ingawa na hofu anaweza kupata pigo la moyo kali sana kwa kuteleza kwenye malezi.
Kwenye jukwaa huru hili kidogo naweza kuwa muwazi, lakini kwa kweli najua waathirika wenzangu wanavyojisikia (kifungoni) baada ya kudhalilishwa huko utotoni kwa namna moja au nyingine...
Mtoto wa kike kubakwa, au wa kiume kulawitiwa ni rahisi kidogo kujulikana...lakini kitendo kama nilichotendewa maana yake nilibeba jukumu kuliko umri wangu ulivyokuwa.
Bahati mbaya, vitendo hivi bado vinaendelea,... na wazazi wakiwa wakali ndio kabisaaaa ...wanakosa kujua yanayowaathiri watoto wao.