USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 12,213
- 28,916
MRADI WA KUCHIMBA VISIMA KATIKA BAADHI YA MAENEO-BIHARAMULO.
Wakati wakazi wa maeneo tofauti tofauti wilayani biharamulo wakisubilia kwa hamu kubwa mradi wa maji wa ziwa victoria bado mbunge wa biharamulo Eng Ezra Chiwelesa anasisitiza na kutilia mkazo uchimbaji wa visima katika baadhi ya maeneo ambayo kwa ramani za mradi wa ziwa victoria inaonesha kuwa kutakuwa muda wa kusubiri hadi maji hayo ya ziwa yawafikie tofauti na maeneo mengine yanayopitiwa na mradi huo mkubwa .
Nguvu ya uchimbaji wa visima virefu inatumika katika baadhi ya vijiji ambapo maji yaliyo chini ya ardhi yanapandishwa kwa nguvu ya umeme au msukumo wa binadamu hadi kwenye vyombo.
Juhudi hizi zinalenga kupunguza uhaba wa maji jimboni katika programu maalumu ya mamlaka ya maji biharamulo kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya na wadau, kila mbinu ya kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana inatumika jimboni na kufikia kiwango cha wastani wa 85% .
Mapambano imara ya mbunge wa biharamulo Eng Ezra Chiwelesa kuhakikisha hoja ya Mh Rais Samia suluhu Hasan ya kumtua mama ndoo kichwani inafikiwa.
AKIAHIDI ANATEKELEZA KUWA SHAHIDI