Chimbo la chupi aina zote

Mkuu Mimi nimekopi na ku paste tu sihusiki na siyajui machimbo ya chupi mi nipo mkoanai huku mwamakiliga Asee😂😂😂

Ni vyema ukaweka location alipo shem wetu wenye uhitaji wamfaate
 
Mkuu Mimi nimekopi na ku paste tu sihusiki na siyajui machimbo ya chupi mi nipo mkoanai huku mwamakiliga Asee😂😂😂

Ni vyema ukaweka location alipo shem wetu wenye uhitaji wamfaate
Kama unaelekea kkoo baada ya kile kituo Cha pili Cha mwendokasi.. mbele kidogo kulia kwako mtaa wa pili unaitwa mahando street humu kuna maduka mengiii ya hzo chupi tight nk..kama uelewi mitaa tafuta kanisa la kkkt la kariakoo... Asa upande wa ubavu wa kushoto wa kanisa ndio maduka yapo mengi tuu na la shem wako...
 
Hii nzuri nikipata mteja mkubwa nitakuunganisha nae awe anachukulia Kwa Shem asee
 
kama ana WhatsApp group la biashara yake tupe link mkuu, itamsaidia shem kukamata vichwa vya mikoani
 
Mbona kama unanishawishi nikafungulie katoto ka 2000.biashara hyo.🤔🤔🤔nipunguze gharama za kumuhudumia.
 
Huyu Dada ANNA CHIMBO sio mkweli hata kidogo na hao Wasaidizi wake hasa kuna mmoja wa Kiume anaafanya biashara hana Customer Care nzuri na anafanya biashara kama karidhika sana, unaweza kumtumia hela akufungie mzigo leo na ukaupata baada ya siku4-5 kwa sababu wanasiku moja tu wameiteua kwaajili ya kufunga na kusafirisha, kosa la pili laa Anna unamtumia sample ya mzigo unaotka lkn atakuchanganyia size usiotaka na aina ya chupi ambayo wewe hukuchagua yaani zile ambazo hazitoki anakuchanganyia ukasumbuke nazo huko, sasa kwa sisi wa mikoani inaumiza maana huna uwezo wa kurudisha unakuta unakula hasara kwa kubaki na chupi nyingi haziuziki na unajikuta mtaji unashuka au unakuwa hupigi hatua, nishaachaga kuagiza kwake maana kila leo msingi unaporomoka kwa kupewa mzigo usiouzika na ukimpigia kumwambia anaishia kuomba msamaha lkn awamu ijayo mambo ni yaleyale
 
Pole sana asee. Mimi Kuna dada kule ndo Huwa anaenda direct kuchagua. Kama nilivyosema kwenye Uzi Mimi siuzagi chupi ila niliunganisha watu
 
Pole sana asee. Mimi Kuna dada kule ndo Huwa anaenda direct kuchagua. Kama nilivyosema kwenye Uzi Mimi siuzagi chupi ila niliunganisha watu
Mwanzo mtaji ulikuwa mdogo kwahiyo niliona ni vyema nikamuamini nikachagua sample anazotuma Instagram kishaa anitumie, siku ya kwanza niliagiza mzigo mdogo maana si unajua hamjuani na unapima uaminifu nashukuru alituma kama zilivyo na nikapiga faida fresh lkn sasa kuanzia awamu ya pili na ya 3 tena ndio nilifungua na tawi mzigo mwingine nikatuma Kanda Maalum huko mzigo ulinikata kila kitu maana mzigo wa hovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…