Chimbuko la Uislam na Karen Armstrong

Kabla hujamalizia, armstrong na wenzie wanawapa nguvu wale waamini wa dhana kuwa dini zote hizi zimeletwa na viumbe wa ajabu kutoka nje ya dunia yetu hii..higher dimensional na kadhalika.

Maana mwanzo wa uislamu kusema mt. Mohammad alivyotokewa na malaika, n.k.

Na zile kauli za mwanzo " na tuumbe mtu kwa mfano wetu"

Haya yote ukijifunza mambo ya elimu ya sayansi ya anga la nje ya dunia na teknolojia zake, utaelewa namaanisha nini.

Kama huna elimu hii, utaniona ni chizi ninayeongea kisichoeleweka.
 
Lakini hayo ya Tuumbe Mtu kwa mfano wetu, Mtume kutokewa na Jibril, ndivyo vitabu vyenyewe vinasema hivyo. So kama waanzilishi wa dhana hii sio sisi au kina Armstrong 'wanadamu' ni mitume wenyewe.
 
Kazi yangu ni moja tu!
safuher

Usisahau kumtag brother Zurri(Sijui anatumia Zurri ipi hata sijui nimtag vipi!)
 
Ingekuwa simple sana unazaliwa tu automatically unamjua Mungu next time Mungu akija kuumba watu uko mbele alifanyie kazi hili jambo.

Maana mabilion ya watu wamekufa pasipo kumjua yeye kama lengo lake katuumba tumuabudu,iwe tu automatically unazaliwa unajua kila kitu kuusu yeye.
 
SEHEMU YA III- MIGONGANO YA UISLAM & DINI ZINGINE ZA KIKURESHI.

Katika miaka ya mwanzo ya harakati zake Muhamad, uislam ulipata waumini wengi ambao walikuwa ni vijana walioumizwa na ubepari wa maka, makundi yaliyokandamizwa kama wanawake na watumwa na koo dhaifu. Ilionekana kuwa, karibu maka yote ingesilimu na kuifuata dini iliyofanyiwa mabadiliko ya al-Lah.

Matajiri na watawala wengi wa maka hawakuwa na shida na dini hiyo, hadi pale Muhamad alipowataka waumini waache kuabudu miungu ya kipagani. Miaka mitatu ya mwanzo ya mahuburi ya Muhamad hakujishughulisha na kusisitiza imani ya Mungu mmoja (al-Lah), hivyo wakazi wengi wa maka waliamini kuwa wangeweza kuendelea kuabudu miungu yao kwa pamoja na al-Lah (Mungu mkuu) kama walivyofanya siku zote. Lakiní alipoanza kuhubiri uharamu wa miungu mingine, alipoteza wafuasi wengi, na uislam adui na kundi la wachache wanaowindwa kuuawa.

Kama ilivyokuwa ukristo wa mwanzo, waislam walichukuliwa kuwa ni wasio Muamini Mungu, kundi ambalo kwa jamii lilionekana kuwa ni tishio. Jamii ya wakureshi ambao 'uumjini' ndio ulikuwa ukiingia, ujio wa uislam ilikuwa ni mgongano wa dhahiri wa kijamii na maisha ya Muhamad mwenyewe yalionekana kuwa hatarini.

Katika jamii ya warabu wa Hijjaz (saudi), kati ya Miungu mitatu, miungu ya al-Lat(Mungu wa kike) na al-Uzza(Aliye Mkuu) ilikuwa ikihusudiwa na jamii hiyo. Al-lat madhabahu yake yalikuwa katika eneo la Taif na Al-Uzza ilikuwa Nakhlah[yote kwa ujumla ilikuwa kusini mwa maka] na Mungu wa tatu, Aliyeitwa Manat (Mungu wa hatma) madhabahu yake yalikuwa Mji wa Qudayd, Pwani ya bahari ya shamu. Miungu huu haikuwa na 'ukamilifu' na iliitwa banat al -Lah (watoto wa kike wa Mungu). Waarabu walikuwa wakitumia neno banat kuonesha uhusiano uliopo kati ya mungu huyo na kazi yake fulani aliyo na nguvu ya kuitenda. Hivyo wanapotumia Banat al-dahr(ni mungu mwenye uwezo wa kuamua hatma). Walipokuwa kuwa wakitumia Banat al-Lah walimaanisha Mwenye Uungu.

Miungu yote hii, kwenye madhabahu, haikuwa na masanamu maalumu bali ni mawe makubwa yaliyosimamishwa. Mawe haya ni mithili ya yaliyokuwepo wakati wa wakanani wa kale, hivyo waarabu waliyatumia kwa ajili ya kuabudia. Kama ambavyo ilivyokuwa kwa kaaba, taif, Nakhlah na Qudayd maeneo haya yalikuwa na umuhimu mkubwa kiimani kwa waarabu. Mababu wa mababu zao waliabudu maeneo hayo na waliamini kuwapa hisia za uponyaji. Uwepo wa Miungu hii ulimpa mivutano na wakureshi, lakini kamwe hakutaka kukubaliana na miungu hii mingi. Jambo kuu Muhamad ambalo alipingana na wakureshi ni kuabudu miungu. Mahubiri yake yote ilikuwa ni msisitizo wa kuachana na miungu yote na kuwa na utii kwa Mungu mmoja (al-Lah) pekee. Kama ilivyosemwa kwenye Sura ya 109 ya Quran; Sema: Enyi makafiri. Siabudu mnacho kiabudu, Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnacho abudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.

Hivyo waislamu watakuwa na utii kwa Allah tu na si kitu wala mila zingine zozote. Kuamini miungu mingine yoyote ilikuwa ni Shirk, dhambi kuu kuliko yoyote kwenye uislam. Wakureshi walisisitizwa kuacha kuabudu mali au utajiri na matajiri na miungu kwani haina nguvu kama al-Lah naye ndiye muweza wa kuwapa kila kitu. Kama ambavyo iliteremshwa kwenye Sura ya 112 ya Quran (Ikhlas) Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee; Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. Muhamad alijua kuwa Imani ya mungu mmoja itatibu ukabila. Hivyo ingeweza kuunganisha jamii na mtu mmoja mmoja. Wakati Wakristo wanasilimu na kuwa waislam, Muhamad hakuwashawishi wajiunge na uislam labda kwa hiari yake mwenyewe. Muhamad mwenyewe aliamini kuwa Wakristo na wayahudi wao tayari walishafunuliwa dini zao halali kwa ajili yao. Kwa Muhamad, ujio wa Uislam hakuwa kwa ajili ya kufuta dini zingine na matendo ya mitume wengine bali ni muendelezo wa dini kwa mwanadamu.

Koran inafunza kuwa Mungu ametuma mitume katika kila kundi la watu hapa duniani na mtume wake. Kama ambavyo imesemwa kwenye Quran (sura ya 2, Al Baqar};
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.

Hivyo Quran, imewataja mitume ambao walikuwa wakijulikana kwa waarabu kama Abraham, Nuhu, Musa na pia Yesu, waliokuwa wakijulikana na waarabu kuwa ni mtume wa wakristo. Pia inawataja mitume wa kale wa kiarabu kama Hud na Salih ambao walitumwa kwa jamii za kale za kiarabu za Midian na Thamood.
 
SEHEMU YA IV- CHANZO CHA KIBLA KUWA MAKA.

Baada ya mikwaruzano ndani ya wakureshi juu ya Uislam na kuabudu mungu mmoja, maisha ya waislam na Muhamad mwenyewe yakawa hatarini. Watumwa na waliochwa huru waliuliwa wakati mwingine na ukoo wake Muḥammad mwenyewe wa Hashim (Hashemites). Waarabu wa kipagani wa Yathrib (ambapo baadae waislam wakaja uita Madina), waliwakaribisha wakaishi kule. Wayathrib ni jamii iliyokuwa imevurugika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na walikuwa kwenye mtanziko mkubwa wa kijamii. Hivyo waliona Uislam kuwa ungewapa muelekeo mpya kiimani na kisiasa. Hivyo waliuhitaji Uislam. Katika jiji hili la Yathrib wayahudi walikuwa ni jamii yenye watu wengi na walikuwa wameshaanza wazoesha wenyeji pale juu ya kuabudu Mungu mmoja. Hii maana yake Muhamad asingepata kazi kuwashawishi juu ya Mungu mmoja kama ilivyokuwa kwa wakureshi. Mwaka 623, Muhamad na familia zipatazo 70 ziliondoka kwenda kuhamia Yathrib (Hijjra).

Baada ya misukosuko ya wakureshi, Muhamad aliona haja ya kushirikiana na jamii ambayo imeshajiimarisha zaidi, hivyo aliusogeza karibu zaidi uarabu na uyahudi. Aliwashawishi waislam kufanya ibada ya funga katika siku takatifu ya wayahudi (Yom Kippur), aliwaagiza wasali mara tatu kwa siku kama wafanyavyo wayahudi (badala ya mbili kama walivyokuwa wakifanya), aliwaruhusu kuoa wanawake wa kiyahudi na kufuata baadhi ya mafundisho/sheria za kiyahudi, Na pia waislam walipaswa kusali kuelekea[Kibla] Jerusalem kama walivyofanya wayahudi. Hivyo wayahudi wa Yathrib (madina) waliiwapokea na kuishi nao vizuri waislam. Lakini baadae waliwageuka na kuanza uadui.

Wayahudi walikuwa na sababu kuu ya kisiasa ya kuwageuka waislam. Walitishika na uwepo wao kwa kuona maslahi yao yako hatarini kutoka kwa waislam hawa wakuja. Wayahudi walianza kumpiga Muhamad na mafundisho yake na kuna nyakati walimdhihaki kuwa iweje mtume wa Mungu anashindwa kujua farasi wake yuko wapi pindi akipotea. Kugeukwa na wayahudi kulimfanya Muhamad avunjike sana moyo na hata kufikiria mara mbili juu ya uelekeo wake kiimani. Lakini si wayahudi wote waliomchukia. Wapo waliompenda na kumpa maandiko ya kiyahudi na kuweza kujisomea. Katika kujisomea maandiko ya kiyahudi ndiko alikojifunza mengi. Kwa mara ya kwanza Muhamad alijifunza mtiririko wa mitume wa kiyahudi na kikristo. Kinyume na alivyokuwa akidhani, alijua kwua wayahudi na Wakristo ni watu wasio dini moja na wasiolewana. Katika mafunzo ya wayahudi aligundua pia, wayahudi wenyewe ni watu walioitwa 'wasio imani' sababu waligeuka na kuabudu sanamu la ng'ombe. Kupitia marafiki wa kiyahudi, Muhamad alijifunza kwenye maandiko yao kisa na Abraham, Isaac na Ismael. Kwenye biblia kisa hiki kinaelezwa kuwa Abrahamu alizaa na kijakazj wake kijana aliyeitwa Ismaili. Baadae mkewe Sarah alizaa kijana aliyeitwa Isaac. Sarah aliamua kumfukuza Haga na mkewe. Mungu kumpa faraja Abarahm alimuahidi Abraham kuwa mwanaye Ismail atakuwa baba wa taifa kubwa. Waarabu pia wana upande wao wa kisa hiki kilichokuwepo miaka mingi kabla ya Muhamad. Wao wanasema kuwa Abarahm aliwaacha Hagar na Ismaili kwenye bonde la mtoto zamzam lililopo Maka na kuwaacha chini ya ulinzi wa Mungu. Maji haya ya zamzam ndiyo yalimnusuru Ismaili na kiu. Baadae Abraham alipoenda watembelea hapo maka, ndipo walipojenga hekalu la Mungu, kaaba. Hivyo kwa waarabu ismail ndio baba wa taifa lao kama ilivyo ismaili kwa wayahudi. Muhamad aliona njia nzuri ya kisa hiki na ufahamu wa waarabu juu ya Kaaba iliyopo Maka, na kuamua kuufanya rasmi uislam uendane na mizizi ya wahenga wa kiarabu. Hivyo hadi kufikia mwaka 624 ilikuwa dhahiri kuwa wayahudi wa madina walikuwa ni maadui wa kudumu wa Muhamad, hivyo January 624 alitangaza rasmi uhuru wa dini mpya ya al-Lah (Uislam). Kutimiza hili aliwaamrisha waislam wabadili kibla kutoka Jerusalem na waelekee Maka. Kubadili kwa kibla ndio linaloitwa tukio la kibunifu zaidi la Muhamad kwenye uislam. Kwani hapa aliufanya Uislam kuwa dini huru kutoka kwenye Ukristo na Uyahudi na wanajimilikisha kwa Mungu, kama alivyofanya abraham alipojenga nyumba yake takatifu ya kaaba pale maka.

Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.

Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake
 
Kuna kitu najiuliza kuhusu idadi ya sala kwa waislamu,nataka kujua sala ni mara tano kwa siku au mara mbili kwa siku? , manake ktk sehemu yako ya PILI ya mada hii umeeleza kusali mara mbili na pia kuna aya kwenye Quran zinaongelea kuhusu kumsujudia mola mara mbili.
 
Kabla ya kiza kuingia nilijua wazi kuwa wale waarabu wa tandale na magomeni wenye ngozi nyeusi, pua pana, nywele ngumu na lips pana watakuja kujambia hii mada

Hiyo ni kwasababu wengi wao wameshashiba kahawa na kashata

Wabillah Tawfiq
 
Mwanzoni zilikuwa mbili. Baadae katika kuwaridhisha/kuwashawishi/kutafuta kukubalika kwa wayahudi waliompokea Madina, Muhamad aliamrisha ziwe tatu kuendana nao. Sasa zilifikaje tano. Tuendelee na usomaji hapa.
 
Uzi hujaisha mkuu,
Teundelee kufuatilia
 
Hii ndio maana ya kutupa akili ya kuchanganua mambo.
Wanyama ndio Wapo hivyo
 
Ukipata kitabu kinachoelezea chimbuko na evolution za imani na dini za kiafrika kichambue pia

Inaboa kuchambua na kujadili imani za kigeni kila siku
Naunga mkono hoja, maana kama Mungu alisema amewatuma wajumbe ktk kila jamii basi nasisi tuwatafute mitume yetu ya kiafrica
 
SEHEMU YA V

A. HIJJA

Mwaka 620 Muḥammad alifanikiwa kurudi nyumbani kwao, mji wa Madina na alipokelewa pasi na tabu yoyote. Mwaka 632 aliwatembelea waarabu wa Hajj waliokuwa wapagana na kusilimisha kuwa waislam. Kwa waarabu, kutembelea Hijja ilikuwa ni utamaduni wao wa miaka mingi kabla Muhamad na uislam haujaja. Ziara hii ya Muhamad, waislam waliipa hadhi na Muhamad kuamuru, kutembelea Hijja iwe ni nguzo ya 5 ya waislam wote.

Waislam wote wana wajibu, wakiwa na uwezo, kutembelea hijja mara moja kwa katika maisha yao. Tukio hili kwa waislam ni kumbukumbukwa Muhamad, lakini tukio hili linamkumbuka pia Abarahm, Hagar na Ismael. Lakini kwa uhalisia zaidi, mamia ya wanaoenda Hijja leo sio waarabu, lakini waislam hawa wamefanikiwa kuufanya Utamaduni wa kale wa waarabu kuwa ni wa kwao. Kama ambavyo wanavyokutana kaaba, waislam huhisi kuwa wametua mizigo yao yote na eneo hili hata kama ni maadui, hapa hawapaswi kukwaruzana.

B. HAKI ZA WANAWAKE.

Wakati wa Uhai wa Muhamad, moja ya kundi alilokuwa akiwapa kipaumbele sana ilikuwa ni wanawake. Katika jamii za waarabu, kabla ya Uislam (jahiliyyah), zilitawaliwa sana na mfumo dume. Wanawake walichukuliwa kama daraja la pili, vichanga wa kike waliuliwa, hawakua na haki ya kumiliki mali, na polygamism Na wanawake walipaswa kuishi kwa baba zao tu hadi watakapoolewa. Uislam ulipiga marufuku kuuliwa vichanga wa kike, iliwaruhusu wanawake kumiliki mali na haki ya talaka. Muhamad aliwapa msisitizo wanawake washiriki katika shughuli za jumuiya (ummah). Wanawake wa Madina mara nyingi walikuwa wakimkibilia Muhamad katika masuala mbalimbali yanapowatatiza. Mfano, walikuwa wakwikwazika kwanini Quran inawasemea wanaume tu hata pale wanawake wanapokuwa wamejiunga n Uislam. Kufuatia hili, Muḥammad aliteremshiwa sura maalum kwa ajili ya kuelezea masuala ya wanawake. Hadi Muhammad anakufa aliacha maandiko yanayosemea haki za wanawake. Lakini baada ya kifo chake, mfumo dume ulishika hatamu kwenye uislam.

So far, hayo ndio mazingira ambayo uislam ulianzia hadi kufa kwa Muhamad, muasisi wake. Sasa unapoutazama Uislam, upo sehemu kuu mbili. Moja ni Mazingira ya Uarabuni kabla ya Uislam hadi kuibuka kwa uislam wenyewe na Pili ni Uislam baada ya kifo cha Muhamad. Baada ya kifo cha Muhamad, mgogoro mkubwa ilikuwa ni nani awe kiongozi wa waislam. Wapo walioamini na walikuwa wengi kuwa aliyepaswa kuwa kiongozi ni Abu Bakar alikyekuwa ni mfuasi wa karibu wa mtume na baba mkwe, hawa walichagua anafaa kwa sababu ya sifa zake(hawa ndio waliitwa Wasuni). Na kundi la pili waliamini kuwa Kama Muhamad angekuwa hai, basi angemchagua Ali, aliyekuwa ni binamu yake. Hivyo, hadi Ali aliposhika uongozi wa uislam(Khalifa), baada ya viongozi watatu kupita, Ndipo baadhi ya waislam walimtambua kuwa ndio Khalifa wao wa Kwanza, hawa ndio washia. Kwa idadi wako wachache duniani. Kuna maelezo yanafaa sana kuwaelezea washia na wasuni, nitayaambatanisha hapa chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…