Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,884
- 5,235
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA VI- SUNNI &. SHIA
A. Sunni.
Jina hili lilitoka na Al Sunna maana yake (wafuasi wa tamaduni i.e mila na desturi za Quran na mafundisho ya Muhamad). Wakati Muhamad amefariki, vigogo walioketi kumteua mrithi walimteua aliyekuwa mfuasi mkubwa wa Muhamad na pia baba wa mke wa pili wa Muhamad aliyeitwa Abu Bakar kuwa ndiye anafaa kuwa mrithi sababu ana elimu kubwa ya uongozi na alikuwa na Busara sana (to me naona ni hoja ya msingi). Waislam wengi waliokubaliana na Uteuzi huu. Hivyo kundi hili likaamini kiongozi wa Kiislam [Caliphate (au Khalifa kwa kiswahili)], anapaswa yule mwenye kufuata na kuzijua Mafundisho ya Muhammad na Quran, kundi hili liliitwa Sunni (wasunni), walikuwa wengi, na hadi leo duniani linahusisha karibu 80+% ya waislam wote duniani.
Nchi nyingi duniani ni Sunni Muslim ( kama nilivyosema hapo juu 80+%). Kwa M.E nchi za Egypt, Jordan, Saudi Arabia, Uturuki na Syria.
B. Shiite/ Shia ( Shiat al Ali - Part/descendants of Ali). -(Washia).
Lakini kapo kakikundi kadogo kalikopinga Abu Bakar kuwa Mrithi wa Muhamad, na kiongozi wa Waislam. Hawa walitaka Ali ibn Talib awe mrithi. Huyu alikuwa ni Binamu wa Muhamad na amemuoa mtoto wa Muhamad aitwaye Fatma. Hivyo wao msimamo wao ni kuwa mrithi alipaswa atoke kwenye damu (ukoo) wa Muhamad mwenyewe-bloodline, kama ilivyokuwa utamaduni wa Kiarabu. Ikumbukwe kuwa Ali, alikuwa ni mmoja wa baraza la vigogo walioshiriki kikao cha kumteua mrithi wa Muhamad kilichompitisha Abu Bakar. Hivyo hawa hawakumtambua Abu Bakar kama Kiongozi wao, hadi mwaka 634, Ali alipokuwa Khalifa baada ya Abu Bakar kufariki. Duniani washia wako kama 10+ %.
Ndani ya M.E Nchi za Iran(90+), Iraq (60+), Bahrain(70+%), Azerbaijan(80%) ndio zenye idadi kubwa zaidi ya washia duniani. Lebanon and Yemen pia takribani nusu ya idadi yao ya watu ni washia. Pia nchi za Saudi Arabia (est 5-10%), Kuwait (abt 36%), Oman(
Lakini pia nao wamegawanyika zaidi. Na migawanyiko hii kwa kiasi kikubwa imetokana na waumini kuwa wafuasi wa wanazuoni fulani fulani wa kiislam (maulamaa) kutoka kwenye madhehebu hayo ya Sunni au Shia
Sunni na Migawanyiko yake:
Hapa licha ya kukubaliana kuwa Khalifa ni lazima atokane na muislam mwenye sifa, lakini hutofautiana kuhusu mafundisho ya sheria za Kiislam. Hapa yapo Makundi Manne, Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali.
Hawa
[emoji830]Wahanafi.
Hawa ni wafuasi wa mafunzo ya Imamu(mwalimu) Abu Hanifa an-Nu‘man aliyezaliwa Iraq na kuishi Iraq miaka ya 700, mafunzo yake yanafuatwa sana huko Asia ya kati, Afghanistan, Pakistan, maeneo ya Levante (Lebanon, Syria, Iraq, Palestine, and Jordan) India, Bangladesh, Northern Egypt na Turkey, Pia waislam wengi wa Urusi ni wafuasi wahanafi. Pia waislam waliopo nchi za Balkan (slovenia, Croatia, Bosnia and Herzegovina, Serbia, Montenegro, Albania, Macedonia, Greece, Bulgaria and Romania.)
[emoji830]Wamaliki.
Hawa ni wasunni wanaofuata mafundisho ya Imam Malik Bin Anas, aliyekuwa mtu wa Madina miaka ya 700 pia. Mafunzo yameshamiri maeneo ya North Africa, West Africa, the United Arab Emirates, Kuwait, baadhi ya maeneo ya Saudi Arabia na Kaskazini mwa Misri.
[emoji830]Washafii.
Hawa ni wasunni wanaofuata mafunzo ya Imam Muhammad ibn Idris ash-Shafi'i mzaliwa wa Gaza, aliyeishi miaka ya 800. Mafunzo yake ni maarufu Huko Hejaz Saudi Arabia, Mashariki ya Misri, Indonesia, Malaysia, Jordan, Palestine, Singapore, Filipino, Somalia , Thailand, Yemen, Kurdistan, Pia baadhi ya waislam wahindi. Nchini Iraq na Syria pia wako kwa kiasi kikubwa.
[emoji830]Wahanbal
Wasunni hawa, hufuata mafunzo ya Ulamaa, Ahmed Bin Hanbal (Jina lake kamili ni Abū ʿAbdillāh Aḥmad ibn Muḥammad ibn Ḥanbal Ash-Shaybānī, kifupi Ibin Hanbal), aliyeishi karne ya 19 kutoka Iraqi (kumbuka Iraq Wasunni ni wachache). Wafuasi hawa wako zaidi Saudi Arabia, Qatar pia kwa uchache wako Iraq na Syria. Mafunzo ya Hanbal ni ya kiitikadi kali na yana mafungamano na Jihadi.
Note: Pia wafuasi wa Salafi ni hufuata mafunzo ya Hanbal. Salaf ni neno maana yake wahenga/waasisi. Hii ni harakati katika uislam inayopigania mabadiliko huku msisitizo wao ni kurudi kwenye mafunzo na matendo ya wahenga wa kiislam. Vuguvugu hili kimsingi wanaamini kuwa waislam halisi walikuwa kizazi cha kwanza hadi cha tatu cha waislam (kutoka kwa Muhamad 600+ years hadi 900+ yrs) walikuwa ndio waislam sahihi. Wanachokipigania hawa ni maisha ya waislam yawe katika misingi ya Quran na Sunna (Matendo ya Muhamad). Vuguvugu hili lilianzishwa miaka ya 1800 kupambana na influence ya western culture and education. Pia wanaaminika kuwa influenced na wahabia.
Wahabia. Ni vuguvugu la kiislam la Kisuni linalopigania mabadiliko ndani ya Uislam lilioanzishwa Saudi Arabia na Mohamed Ibn Abd al-Wahhab miaka ya 1700. Hawa wanapigania Mafunzo ya kiitikadi kali ya imani kwa Allah na tafsiri ya Quran na Uislam bila kupindisha neno. Wahabia wanaamini Muislam yeyote asiyekuwa na mafungamano au mtazamo huo, basi huyo ni Kaffir (mchafu/aliyelaanika/asiye Muislam) na ni adui wa Uislam. Vuguvugu hili kwa kiasi kikubwa linapata fedha kutoka kwa Serikali ya Saudi Arabia [ili kueneza dini!!!!] Kundi kama ISIS ni wafuasi/sehemu ya Vuguvugu hili.
Washia na Mgawanyo wao:
Hivyo kama tulivyosema hapo juu, Washia wanaamini Khalifa wao wa Kwanza ni Ali bin Talib. Baada ya hapo wakafuata Makhalifa wengine au pia huwaita Maimam (sababu ni walimu wao kiimani).
Washia wako makundi makuu mawili.
i. Imamiyah au Twelvers.
Hawa ni washia wanaoamini kuwa baada ga kifo cha Muhamad, kulifuata Maimam 12 walioongoza Uislam huku imam wa mwisho, Muhamad Al Mahid aliyezaliwa mwaka 870 huko Abissas Empire (Iraq ya Leo) na kupotea akiwa na miaka mi5 atarejea miaka ya baadae akiwa na Nabii Isa (Yesu) na kuwakomboa walimwengu. Wafuasi wa Kikundi hiki wanapatikana Iran, Iraq, Pakistani, Uhindi, Bangladesh, Shamu, Lebanon, Kuwait, Muungano wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Uarabuni ya Saudia, Burma, Thailand, Indonesia, Urusi, Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Zaire, Malagasy, Ungazija, Uingereza, Marekani. Pia chini yao kuna madhehebu Mengine ambayo yanapingana kuhusu idadi ya hao maimamu, wengine wakiwakataa baadhi ya maimamu.
Hawa ndio 12 Imams;
1. Ali bin Abi Talib
2. Hasan bin Ali
3. Husain bin Ali
4. Ali bin Husain
5. Muhammad bin Ali
6. Jaafar bin Muhammad
7. Musa bin Jaafar
8. Ali bin Musa
9. Muhammad bin Ali
10. Ali bin Muhammad
11. Hasan bin Ali
12. Muhammad bin Hasan (aliyetoweka akiwa na miaka 5 na atagemewa kurudi kuwakomboa).
ii. Ismailiya:
Hawa washia wanaamini kuwa Uimamu baada ya Imamu Jaafar Sadiq [huyo watano hapo juu] ulichukuliwa na mwanawe Ismail.
Maismailiya Wamegawanyika tena katika Madhehebu mawili; Aga Khan na Bohora.
Maagha Khani:
Hawa hufahamika zaidi kwa jina la Maismailiya hapa Afrika ya Mashariki na sehemu nyinginezo, ingawa vitabu vya kidini huwaita Nazariya. Wanamwamini Mtukufu Karim Aga Khan IV kuwa ni Imamu wao wa 49.
Mabohora:
Hawa Wanaamini kuwa Imamu wa 21 yu katika Ghaib (haonekani) na yu hai. Kwa wakati huu kiongozi wa jamii yao anaitwa Mufaddal Saifuddin akiishi Bombay, India.