Niliposikia wahamiaji kutoka bara...nikajua ni bara kweli...wapi..mleta mada anasema wanatokea Kisarawe! Sasa Kisarawe toka lini ikawa Bara. Nina wasiwasi mleta mada ni mzaramo tena mjukuu wa Chifu Pazi (nimemkumbuka Idd Pazi, golikipa matata sana enzi hizo...mpira tunaufuatilia 'Redio Tanzania-Dar es-Salaam'..watangazaji Omary Jongo na Ahamed Jongo na dereva wa OB van nimemsahau jina). Wazaramo kwa 'kukuza mambo hawajambo'. Eti wahamiaji kutoka bara. Ha ha haaa!