Chimbuko la wazaramo

Chimbuko la wazaramo

Hili ndo tatizo la watu wabara,mnaongea mambo sijui mnayatoa wapi.Wazaramo ni wenyeji na wenye mji wa dar es salaam.kuna wazaramo ambao asili yao ni Ilala na wengine msasani.Maneromango,Masaki,Kibuta nk kote ni uzaramoni.
Kuna waamiaji wa Dar wanapenda kuaminisha kuwa Dar ni mkoa wa waamiaji,si kweli wenyeji ndo hao Wazaramo.
 
Niliposikia wahamiaji kutoka bara...nikajua ni bara kweli...wapi..mleta mada anasema wanatokea Kisarawe! Sasa Kisarawe toka lini ikawa Bara. Nina wasiwasi mleta mada ni mzaramo tena mjukuu wa Chifu Pazi (nimemkumbuka Idd Pazi, golikipa matata sana enzi hizo...mpira tunaufuatilia 'Redio Tanzania-Dar es-Salaam'..watangazaji Omary Jongo na Ahamed Jongo na dereva wa OB van nimemsahau jina). Wazaramo kwa 'kukuza mambo hawajambo'. Eti wahamiaji kutoka bara. Ha ha haaa!
 
Hii inaonesha kuwa hakuna mtu mwenye uhakika na kabila lake kiasili.Watu wanapata wapi ujasiri wa kutukana kabila lingine ikiwa huenda kabila hilo asili yake ni kwenu.Tena kabila linaloongezwa kwa kudharauliwa ni wazalamo. Kila kabila likichambuliwa utamaduni zao itakuwa hatari.
 
Back
Top Bottom