Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha: Fang Bin
Fang alipotea mara tu baada ya kushea video na picha zilizoonyesha hali halisi ilivyokuwa katika Mji wa Wuhan, ambacho ndicho kilikuwa kitovu cha Uviko19.
Taarifa zinadai kuwa mwanaume huyo alikamatwa kwa sababu mamlaka husika hazikutaka kutoa taarifa za ukweli kuhusu mlipuko wa Uviko19 ulioleta ‘jinamizi’ kubwa duniani.
Kwa mujibu wa mwanafamilia mmoja, Fang aliachiliwa huru Jumapili iliyopita na hali yake ya kiafya sio nzuri kutokana na matatizo ya kula na kulala yaliyompata alipokuwa kizuizini hivyo kupelekea kupoteza uzito mwingi na kuwa mdhaifu.
Katika moja ya video alizoziposti hospitali za mji wa Wuhan zilionekana zikiwa zimelemewa na wagonjwa pamoja na ndugu zao huku video nyingine ikimuonyesha akihesabu mifuko iliyokuwa imebeba miili ya watu.