Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Serikali ya China imetangaza kufunga shughuli zote za kawaida kwenye mji wa watu takribani milioni 4, wa Lanzhou na kuaamuru watu kutotoka nje isipokuwa kwa dharura, ikiwa ni jitihada ya kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya corona kwa visa vichache vilivyothibitishwa.
Vizuizi hivyo vya leo vinatolewa wakati China ikitoa taarifa ya visa 29 vipya vya maambukizi ya ndani, vikiwemo sita katika mji wa Lanzhou, ambao ni mji mkuu wa jimbo la kaskazini magharibi la Gansu.
Huduma za mabasi ya umma na magari ya kukodi tayari zimesimamishwa katika mji huo, na vyombo vya habari vya umma vinasema mamlaka ya safari za reli ya Lanzhou imesimamisha safari 70 za treni, ikiwemo ya kwenda Beijing na Xi'an.
Mripuko wa hivi karubuni unahusishwa na aina ya virusi inayosambaa kwa kasi ya Delta, inayofanya jumla ya visa 198 tangu Oktoba 17. Na 38 ya visa hivyo vikibainika katika mji Lanzhou.