FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Jana nilikuwa na mazungumzo na mchina mmoja juu ya mgogoro unaondelea baina ya Urusi na Yukrein.
Kubwa kabisa nilimuuliza, ni kwanini uChina haitaki kumchukulia hatua kali Urusi ili kuonyesha kupinga anachokifanya Yukrein ambacho ni kitendo haramu cha uvamizi?
Akajibu kwamba anachofanya Putin ni sahihi kwa sababu intelijensia ya Uchina na Urusi imeonyesha kwamba Marekani ina mpango wa kurudisha tena silaha za nyuklia nchini Yukrein ambayo kabla ya kuvunjika kwa umoja wa Kisovieti , ilikuwa ni sehemu ya Urusi. Mpango huu unaenda sambamba na kuijumuisha Yukrein katika umoja wa kujihami wa nchi za Ulaya (NATO) ambapo baada ya kujiunga nayo, NATO ambayo kiranja wake asiye rasmi ni Marekani, ina kuwa na uwezo sasa wa kuingiza silaha za aina mbalimbali katika himaya za nchi mwanachama aliyejiunga kwa madhumuni ya kuimarisha ulinzi wa kujihami, silaha za nyuklia zikiwa mojawapo.
Akasema, kitendo hicho kinamuogopesha sana hasimu mkuu wa Marekani tangu kipindi cha vita baridi iliyodumu kwa miongo kadhaa baada ya vita kuu ya pili ya dunia, naye si mwingine bali ni Urusi, ambapo inakuwa ni kama adui yake ameleta silaha za nyuklia uwani kwake, kitu ambacho Putin hawezi kukubali kamwe. Anasema, tangu 2008 , Urusi imekuwa ikiipa Yukrein maonyo makali sana juu ya mpango wake huo wa kutaka kujiunga na NATO, lakini nguvu kubwa waliyonayo mabeberu ikiwemo misaada na marupurupu mengine mengi yaliifanya Yukrein imgeuzie kisogo Urusi na kuegemea upande wa mabeberu, na hivi karibuni lile vuguvugu la kujiunga na NATO ndio lilipamba moto sana.
Sasa kwa mujibu wa NATO, ni kwamba ukaigusa nchi yeyote ile ambayo ni mwanachama wake, hiyo ni sawa na kuivamia ulaya yote, maana yake ni kwamba nchi zote za ulaya na wanachama wa NATO, Marekani ikiwemo, watajibu mapigo kwa haraka na kwa uhakika, mercilessly!!, ndio maana Urusi hathubutu hata kurusha jiwe kwenda Poland ambayo ni mwanachama. Sasa ili kuepusha vita kuu ya tatu ya Dunia, Putin akaamua kuiwahi Yukrein kabla haijajiunga na NATO, maana angejiunga tu, ndio ingekuwa mwisho wa mchezo, asingeweza hata kurusha mkuki achilia mbali kombora kwenda Yukrein. So in essence, huu ni mwendelezo wa ‘Proxy wars’ baina ya Urusi na Marekani kama ile ya Syria, Vietnam nk; ni vita ambazo mabeberu wanapigana kwa remote control, ila wanaokufa ni raia wa nchi zingine, wao kazi yao ni kutoa misaada ya silaha tu ili muendelee kupigana, hata ISIS walipewa silaha za kutosha tu ili kumg’oa Bashar Al-Assad, lakini kwakuwa Urusi nayo ilikuwa ikimpa sapoti ya silaha na kifedha Assad, basi hadi leo wamegonga mwamba.
Akaniambia hata Taiwan ilikuwa sehemu ya Uchina, na katika hili vuguvugu la sasa, kuna hamu na mnyevuo mkubwa ndani serikali ya Uchina, kutaka kuikwapua Taiwan ili kuirudisha chini ya himaya ya Uchina, na mipango yote imefikia hatua nzuri sana...
Pia akasema kwa dunia ya sasa, vita kubwa zaidi ni vita ya ki-propaganda, ambapo mabeberu wa magharibi wameshika mpini na Urusi imeshika makali, maana mitandao mikubwa ya kijamii yote imeshikwa na mabeberu hayo, ikiwemo Facebook, Instagram, Youtube, twitter, google NK, ambapo ukadiriki tu kutoa mtazamo kama huu juu ya mgogoro huu, basi moja kwa moja utapoteza akaunti yako, hata sattelite TV nyingi zipo mikononi mwa mabeberu, na mwanzo mwisho wanatapika propaganda za kibeberu tu...
===============================
www.theguardian.com

China could mount full-scale invasion by 2025, Taiwan defence minister says
Comments come as Biden and Xi agree to stick to Taiwan agreements amid rising tension in Indo-Pacific