China Kufadhili Ujenzi SGR Mwanza -Isaka

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ambao unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyia kazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.

Pia, soma: Kwanini ujenzi wa SGR hapa Mwanza umesimama?

Dkt. Nchemba amesema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Balozi Chen kwamba China kupitia Taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, amesema kuwa Nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo Afrika.

Amesisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.

Amesema mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

View attachment 3119766
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akiwa na ujumbe kutoka ubalozi wa china nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa. Kushoto ni Bw. Chu Kun na kulia ni Katibu wa Balozi, Bi. Ma Shukun.
Marehemu si aliisha Acha ame sign hicho kipande. Maana alijua wahuni wana mpango wa kutoiendeleza hiyo reli
 
Kwahiyo wale wanaojenga wanajenga bila hela? Hii ilisainiwa Waziri wa ujenzi akiwa Dr. Chamuliro. Enzi za JPM. Kumbe hawana hela
 
Habari imekaa kisiasa zaidi,

Ujenzi umefika % ngapi na ufadhili ni pesa ngapi mchina atatoa?

Ujenzi ulishaanza enzi za JPM. Hata leo ukienda Mwanza, Butimba kuna foleni sababu ya Ujenzi wa SGR. Huyu mwamba anatuletea picha eti wanafadhili ujenzi wa Mwanza Isaka.
Kwani kuwa mwana siasa lazima uwe muongo? Na unamdanganya nani saSA?
 
Tumehamia Asia sasa hivi kutembeza bakuli? Tutegemee Wachina kuajiliwa kwenye SGR kama watu wa Uendeshaji na Utawala.
Tanzania Tanzania tunakupenda lakini Watawala wameamua kukugeuza na kukuchezea tu. 😭😭😭😭
Bado viongozi wetu hahawajui wachina vizuri! au ndio wanajifanya hawasikii?
 
Zambia mpaka Trafiki ni Mchina kwa sababu ya kuendekeza mikopo na kushindwa kupeleka marejesho. Na sisi tutafika mpaka huko hawa Mama Kizimkazi na huyu Mnyiramba wakiendelea kukalia viti hivyo
 
Utapiga Ramli mpaka utachoka.
 
Mh hivi tuliopisha mradi na tunaosubiri kulipwa fidia za sgr tutalipwa kweli?
 
Ndio mtalipwa kwa haki kabisa bila kudhulumiwa hata shilingi mia.
Tathmini toka mwez wa tatu had Leo kimya watu tukakopa Ili tumalizie ujenZi wa makazi mapya Ili tukilipwa tuhamie kwetu badala ya kupanga na tuwalipe wadeni wetu lkn had Leo wadeni wetu wametununia
 
Kuweni na subira ndugu zanguni.kama mnavyojua kuwa pesa ya serikali inakuwa na taratibu zake za utokaji.lakini muwe na imani ya kuwa hakuna atakaye dhurumiwa
 
Back
Top Bottom