China Kufadhili Ujenzi SGR Mwanza -Isaka

China Kufadhili Ujenzi SGR Mwanza -Isaka

Huna hata aibu,kwani nchi hii Haina engineers,rasilimali zote hizi Bado ccm wanakopa.ujinga²⁷
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR ambao unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyia kazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.

Pia, soma: Kwanini ujenzi wa SGR hapa Mwanza umesimama?

Dkt. Nchemba amesema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Balozi Chen kwamba China kupitia Taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa Nchini, Chen Mingjian, amesema kuwa Nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo Afrika.

Amesisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.

Amesema mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

View attachment 3119766
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akiwa na ujumbe kutoka ubalozi wa china nchini, wakimsikiliza Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa. Kushoto ni Bw. Chu Kun na kulia ni Katibu wa Balozi, Bi. Ma Shukun.
kumbe ujenzi kati ya mwanza na isaka umesimama huku wnasema mama anaupiga mwingi? Kipaumbele kinatakiwa kiwe huu ujenzi wa miundombinu. Sio kuwapa wahindi na waarabu kuendesha miradi taifa limewekeza halafu mnaambia watu eti ni uwekeaji.
 
Yote kheri, cha msingi ni namna gani tunaenda kusimamia miradi hii ili ituletee tija. Nje ya mada : - Ile ndege yetu ya mizigo inafanya nini kwa sasa? Mara ya mwisho walizenguana na Kenya wakigombea mizigo ya Kenya
 
Rais sasa hivi ni Magufuli ama Samia Suluhu!?
Tunauomba jibu tafadhali.
Kwani hizo fedha alizosema zipo aliondoka nazo? Kwani alikuwa anatoa mfukoni mwake? Kwani hazina haipo? Kwani alivyosema hivyo alikuwa ameangalia fedha kwenye account yake au ya hazina?
 
Kwani hizo fedha alizosema zipo aliondoka nazo? Kwani alikuwa anatoa mfukoni mwake? Kwani hazina haipo? Kwani alivyosema hivyo alikuwa ameangalia fedha kwenye account yake au ya hazina?
Mbona unajiuliza na kujijibu mwenyewe!?
Unajivuruga,Samia amekopa mara tatu ya watangulizi wake wote,swali linakuja,mtangulizi wake aliwezaje kujenga bila kukopa hovyo kama yeye!?
 
Mbona unajiuliza na kujijibu mwenyewe!?
Unajivuruga,Samia amekopa mara tatu ya watangulizi wake wote,swali linakuja,mtangulizi wake aliwezaje kujenga bila kukopa hovyo kama yeye!?

Tustick kwenda hoja:Serikali hii inayoongozwa na Sir1oo haina tofauti na JPM kwasababu sir100 alikuwa Makamu wa Rais ,kwahiyo Serikali yao wakati wanaanza ujenzi walisema kwamba wanatekeleza miradi kwa fedha za ndani ,miradi ilikuwa ya serikali na si ya JMP au Sir100 kwasababu fedha ilikuwa haitoki kwenye personal accounts zao bali hazina.
 
Nime stick kwenye mada ila yaonekana unakaza fuvu.
Niletee ushahidi wa mkopo wa phase 1 wa SGR!??
Ushasema makamo wa Rais.
Je Samia kuwa makamo wa rais ndio justification akiwa rais atakua sawa na Magufuli!?
Mbona alivyoingia madarakani kuna reforms kibao amefanya na kupinga sera za Magufuli!?
 
Back
Top Bottom