kama ulivyo elezwa hapo juu, ila nitaongezea kidogo.
kuna faida kama mbili tatu za thamani ya fedha ya nchi fulani kuwa chini.
1. export, hapa kwenye ku export ni kwamba waagizaji wana agiza katika bei ya chini na wao wanaenda kuuza kwenye nchi zao bei ya juu so tiyali wanakuwa wametengeneza faida
2. kwenye ku utract investers, nazani hili ndo nalo lina sumbua nchi za ulaya, nchina kuna foleni ya wawekezaji wengi sana wanao kimbilia huko mfano wawekezaji kutoka, japani, marekani na ulaya, so fedha ya nchi ikiwa chini wawekezaji wanapata unafuu kwenye, ghalama za ku invest, pamoja na ghalama za kuwalipa mishahara wafanyakazi so mwekezaji akichenji dola zake kwa fedha ya china tiyali atakuwa na fedha za kutosha kuinvest china.
3. Kitu kingine kinacho ipa china unafuu ni population yao, pamoja na fedha yao kuwa chini still population yao inawabeba sana- investers wengi wanakimbilia china kwa sababu wanajua soko la ndani lenyewe ni kubwa kuliko hata soko la nje
- kwa huku bongo pamoja na kwamba fedha yetu iko chini sana haiwezi vutia wawekezaji na exportation kwa sababu zifuatazo.
1. urasimu kwenye uwekezaji ni mkubwa sana
2. low purchasing power ya nchi yetu, bado purchasing [power yetu iko chini sana so wawekezaji mathalani hawawezi kuja kuwekeza kiwanda cha kutengeneza magari huku wakifahamu fika wanunuzi ndani ya nchi watakuwa wachache sana
3.miundo mbinu yetu, barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari ni vikwazo tosha vya kwa nini pamoja na fedha yetu kuwa chini bado hakuna wawekezaji wano vutiwa
4. mambo ya upatikanaji wa umeme, maji na kazalika nayo yanachangia kwa sana
5. financial systeam zetu bado ziko nyuma sana.
6. Na population yetu nayo ni kikwazo, ila kwa sasa kwa sababu ya jumuia ya africa mashariki kidogo wawekezaji watavutiwa na population kuwa kubwa.
7. Hata huko rwanda ambako wanadai wawekezaji wanakimbilia ni wanawekeza kwenye biashara kama huku bongo tu, pombe, mafuta ya kula, kujipaka. Sabuni, na kazalika.
- NA HATA HIVYO HATUNA CHA KUUZA NJE YA NCHI NAAMANISHA KWENYE MASOKO YA ULAYA, MAREKANI NA ASIA, SANASANA NI MADINI, NA LOW MATERIO AMBAZO ZINAUZWA BEI CHEE KWA SABABU HATUJA VIONGEZEA THAMANI YEYOTE ILE.
- NA TUKISEMA TUUZE SOKO LA AFRICA MASHARIKI NAO NI UONGO, WANAVYO ZALISHA KENYA NDO TANZANIA WANAZALISHA NDO UGANDA WANAZALISHA
- ndo maana wawekezaji wengi wanao wekeza tanazania wanawekeza katika bidhaa ambazo si ghali sana mfano kwenye-
1 viwanda vya pombe- hapa wanunuzi ni wengi sana
2. Viwanda vya sabuni, mafuta na kazalika.
3. Na tourism industry na hii inavuta wawekezaji wengi kwa sababu wanunuzi c watanzania bali ni wazungu wenzao
kwa hivi viwanda vya huku kwetu hata siku moja tusidhani tuta compete international, leo hii nchi kama south africa inaweza compete na nchi za ulaya kwa sababu wana viwanda vikubwa vya kutengeneza mitambo mbalimbali na c viwanda vya pombe na sabuni