China kutengeneza mwezi wa bandia

China kutengeneza mwezi wa bandia

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Katika jitihada za kupunguza gharama za taa za barabarani usiku, jiji la Chengdu nchini China litakuwa na kivutio kikubwa cha utalii katika mpango wake wa kutengeneza mwezi wa bandia utakaowekwa angani.

Mwezi huo wa bandia, ambao utaongeza mwanga wa mwezi halisi wa sasa, unatarajiwa kuwa umekamilika ifikapo mwaka 2022, gazeti la China la People's Daily limeripoti.

Gazeti hilo limekariri taarifa ya jarida la sayansi na teknoloji likisema kuwa mwezi huo wa kutengenezwa na binadamu unaundwa na chombo cha setalaiti kilichobeba kioo kikubwa ambacho kinaweza kuakisi mwanga wa juu na kuutuma ardhini.

Kwa mujibu wa mipango ya utafiti wa mradi huo, uthibitishaji wa uzinduzi, kuuweka mwezi huo katika mistari ya orbit, kuuanzisha, kurekebisha na shughuli za usimamizi wa mwezi huo utakamilika mwaka 2020, alisema Wu Chunfeng, kiongozi wa Taasisi ya Utafiti wa Sayansi wa Wilaya ya Tianfu jijini Chengdu. jiji hilo liko katika jimbo la Sichuan lililoko kusini magharibi mwa China.

Miezi mitatu ya kutengenezwa na binadamu itazinduliwa mwaka 2022.

"Kwa wakati huo, vioo vitatu vikubwa vitaigawanya chombo hicho chenye nyuzi 360, kuwezesha kumulika eneo kwa saa 24 mfululizo," alisema Wu.

Mwanga utakaoakisiwa utaweza kumulika eneo la kuanzia kilomita 3,600 za mraba hadi kilomita 6,400 za mraba na ukali wa mwanga huo unategemewa kuwa mara nane ya mwanga wa mwezi halisi, kwa mujibu wa Wu.

Mwezi halisi unamulika dunia kutoka karibu kilomita 380,000, wakati mwezi huo bandia unategemewa kuwekwa kwenye mzunguko ulio ndani ya kilomita 500 kutoka duniani.

Akijiubu swali kama mwezi huo wa bandia unaweza kuvuruga mzunguko wa kawaida wa usiku na mchana kwa mimea na wanyama, Wu alisema ukali wa mwanga unaweza kurekebishwa na usahihi unaweza kudhibitiwa. Wakati mwezi huo utakapokuwa unafanya kazi, watu wataweza kuona nyota ambazo zina mwanga mkali tu.

Mwez huo wa bandia ni muhimu kwa maisha ya kawaida.

"Kutumia mwezi wa bandia kumulika eneo la kilomita 50 za mraba, kunaweza kuokoa gharama za umeme kwa yuan 1.2 bilioni," alisema Wu (yuan moja ni sawa na Sh330.3 za Kitanzania).

"Pia unaweza kumulika sehemu ambazo umeme unakatika kutokana na majanga kama tetemeko la ardhi."
 
Sawa sisi bado tunamtafuta Mo akipatikana tutatengeneza ata nyota ya bandia
 
mwanga wake utakuwa mara nne zaidi ya mwezi wa kawaida. TUNAWEZA KUHITIMISHA KWA KUUPA JINA LA full moon but artificial au Artificial full moon.
 
Ngoja sisi tununue wapinzani mambo mengine baadae
 
Sisi huku tumevumbua leo aina ya nne ya picha sirrophotograph ambayo inakuja kushindana na CCTV Camera's zote ulimwenguni asante sirro
 
Back
Top Bottom