China kutoa uamuzi wa kufadhili ujenzi wa SGR baada ya tathmini kukamilika hivi karibuni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1728645109477.png

1728645207582.png

1728645499146.jpeg

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.

1728645507592.jpeg

Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Mheshimiwa Balozi Chen kwamba China kupitia taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, amesema kuwa nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo barani Afrika.

Alisisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.

Aidha, alieleza kuwa mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

WIZARA YA FEDHA
 
Tatizo la viongozi wa Tanzania hawaongea gharama walio toa kumshawishi China kufanya hivo katika uchumi wa ubepari hamna msaada usio kua na conditions attached. Badaye ndo tutaanza kulalamika hoo mbona wachina ndo wanaendesha SGR yetu.
 
Hatukuwmbiwa kuwa watafadhili?

Hili la kutathmini siyo jipya?

Bongo *yoso!
Mwendazake alisema tunajenga kwa hela za ndani akawafurusha wachina na mkataba wao wa kujenga sgr. Leo tumerudi kule kule. Hivi hawa viongozi hawana aibu? Hawaoni soni wanapoenda kwa hawa wachina kuomba misaada?
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), ameishukuru China kwa kufikia hatua za mwisho za kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaendelea hivi sasa kwa kipande cha tano cha kuanzia Mwanza hadi Isaka na kuahidi kuyafanyiakazi maombi mengine ya kipande cha sita kinachoanzia Tabora hadi Kigoma.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala muhimu ya ushirikiano kati ya China na Tanzania uliodumu kwa miaka 60 sasa.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Mradi wa Reli ya Kisasa ni muhimu kwa uchumi na maendeleo ya Watanzania na kwamba ujumbe wa Mheshimiwa Balozi Chen kwamba China kupitia taasisi zake inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo umepokelewa kwa mikono miwili na Serikali.

Kwa upande wake, Balozi wa China hapa nchini, Mheshimiwa Chen Mingjian, amesema kuwa nchi yake inauchukulia uhusiano wake na Tanzania kuwa ni wa kipekee na kwamba maelekezo ya Kiongozi wa nchi hiyo Mheshimiwa XI Jinping ni kwamba anataka uhusiano huo uwe wa mfano na kielelezo barani Afrika.

Alisisitiza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha kwa ajili ya kipande cha tano na mengine ya kutaka ufadhili wa ujenzi wa kipande cha 6 yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa hivi karibu baada ya mambo machache yanayofanyiwakazi kukamilika.

Aidha, alieleza kuwa mpango wa miaka mitatu wa China wa ushirikiano kati yake na nchi za Afrika (FOCAC), umeitengea Tanzania kiasi kikubwa cha fedha ambazo zitaelekezwa katika miradi inayogusa masuala ya uchumi wa kijani, biashara na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

WIZARA YA FEDHA
Halafu hawa viongozi wetu mbona wanatupiga swaga kuwa kipande cha SGR kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora kimekamilika kwa urefu wa Km. 722 badala ya Km. 535?

Hizi Km. 187 zilizoongezwa zimejengwa angani?

Kwanza kwa nini hawa viongozi wetu wasiseme ukweli kuwa kipande hicho kina urefu halisi wa Km. 535? Au wanatafuta kiki za kuonyesha kuwa fedha za walipa kodi zimefanya kazi kubwa wakati uhalisia hauko hivyo?
 
UCHUMI: Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali ya China inakamilisha taratibu za ndani za kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaoendelea kwa kipande cha 5

Dkt. Mwigulu amesema hayo baada ya kukutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian ambapo Balozi alieleza kuwa maombi ya Tanzania ya kupata fedha yamepokelewa na kwamba uamuzi wake utatolewa baada ya kukamilika kwa mambo kadhaa yanayofanyiwa kazi

Ujenzi wa SGR uliokamilika hadi sasa ni Dar - Dodoma (Kilomita 722), na unaoendelea ni Makutupora - Tabora (Kilomita 294), Tabora - Isaka (Kilomita 130) na Isaka - Mwanza (Kilomita 249)

Soma China kutoa uamuzi wa kufadhili ujenzi wa SGR baada ya tathmini kukamilika hivi karibuni
 
Kenya wametoa airport kwa India tayAri, Africa uchumi hatuwezi achananeni tu tuzidi kuwaza namna ya kuikojoza na namna ya kula Bata na kuuza madini na Wala tunachoweza zaidi ya starehe,njia za uchumi apewe mtu mweupe
 
Back
Top Bottom