mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Seneta na bosi mstaafu wa Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga (NASA), Bill Nelson, ametoa tahadhari kuwa muda wowote China wanaweza kuumiliki mwezi mzima ukawa mali yao.
"tuko katika mashindano ya kianga, na China watajimilikisha mwezi endapo wakafanikiwa kufika huko kwa kisingizio cha utafiti" amesema bosi huyo.
Wanaanga kutoka China wanategemewa kufika mwezini ndani ya Muongo huu mmoja kulingana na gazeti la The New York Times.
Marekani haitaki China kuwa na eneo la kudumu mwezini..yaani China wakatembee tu mwezini lakini sio kwenda kufanya utafiti...kuanza kuchimba chimba.
Ishu iko siriaz..ripoti kiusalama ya mwezi novemba 2022 kutoka Pentagon kwenda kwa bunge/Congress ilieleza kuwa china wataweka kituo mwezini sawa na kituo cha kijeshi chenya uwezo wa "surveillance" / upelelezi/kuScan au kufuatilia dunia nzima kwa undani zaidi...na wakifanya tu hivyo hakuna atakayeweza kuwazuia.
Source: IJR: Article: NASA Chief Sounds the Alarm - Chinese Moon Base May Soon Be Over our Heads