Mwaka huu Chama cha Kikomunisti cha China, CPC, kinatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa.
Mtaalamu wa masuala ya China ambaye pia ni Mhadhiri wa Siasa ya Jamii.
katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Dkt. Otiato Wafula anasema China chini ya usimamizi wa chama cha kikomunisti cha China imezisaidia Nchi nyingi za Afrika Katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu.
Dk Wafula anasema China ni mwenzi na rafiki wa dhati wa Afrika.
Aidha anasema kuwa Nchi za Afrika zinafaa kuiga sera ya ujamaa ya China na kujifunza utamaduni wa China ili kufikia maendeleo makubwa zaidi.