CRI Swahili
Member
- Dec 21, 2013
- 19
- 42
Rais Xi Jinping wa China leo ametoa mwito wa kuendelea kwa juhudi za kupambana na dawa za kulevya. Kwenye ujumbe aliotoa mapema kabla ya maadhimisho ya siku ya kupambana na dawa za kulevya (26 June), Rais Xi amesema msimamo mkali dhidi ya dawa za kulevya ni lazima uendelee, ili kupata maendeleo zaidi kwenye udhibiti wa dawa hizo.
Rais Xi amesema kwa sasa tatizo la dawa za kulevya limefungamana na tatizo hilo nje ya China, na linahusika na uhalifu wa kwenye mtandao wa internet na nje ya mtandao wa internet, na kuhatarisha sana maisha ya watu, afya zao, na utulivu wa kijamii
Akisisitiza msimamo mkali kuhusu tatizo la dawa za kulevya Rais Xi ameziagiza kamati za chama na serikali katika ngazi mbalimbali kuboresha mfumo wa usimamizi kwenye usimamizi wa dawa za kulevya na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Serikali ya China inatumia mbinu mseto kupambana na dawa za kulevya. Njia hiyo inahusisha kuzuia dawa za kulevya kuingia kwenye mipaka ya China na kushughulikia zile zilizo ndani, kufanya ushirikiano wa kimataifa, kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa afya, usalama, uchumi na jamii, na kujenga vituo vya kutoa matibabu ya kuwasaidia wenye uraibu wa dawa za kulevya.
Takwimu zilizotolewa mwaka jana na kamisheni ya kupambana na dawa za kulevya zinaonyesha kuwa asilimia 0.18 ya wachina (takribani watu milioni 2.5) wanatumia dawa za kulevya.