Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Mwaka 2019 serikali ya Marekani chini ya aliyekuwa raisi wakati huo Donald Trump, iliweka sheria ya kutotumia huduma na vifaa vya Huawei katika idara nyeti za usalama wa taifa hilo.
Sababu kuu ilikuwa ni kwamba usalama wa taifa hilo ulikuwa hatarini, ikidai kuwa China inaitumia kampuni ya Huawei kama chombo cha kijasusi.
Pentagon ambayo ni idara kuu ya usalama ya Marekani, ilipewa kazi hiyo ya kuhakikisha kuwa idara zote za kiusalama, huduma za kijeshi, kambi za jeshi la Marekani zilizo ndani na nje ya Marekani, maafisa wa usalama na ulinzi wa Marekani hawatumii huduma na vifaa vya Huawei.
Ikiwa inakaribia miaka 5 tangu Pentagon wapewe kazi hiyo, imeonekama hawajatimiza ipaswavyo jukumu hilo walilopewa na bunge la Marekani.
Ni changamoto gani zimefanya Pentagon ishindwe? Changamoto kuu 6 walizokumbana nazo Pentagon:

- Huawei ni kampuni kubwa ya teknolojia ya mawasiliano ambayo huduma zake zinatawala kwa 40% katika soko la dunia. Hivyo imekuwa vigumu sana kwa nchi washirika zenye kambi za jeshi la Marekani kuachana na Huawei from the scratch.
"Kuna sehemu fulani za ulimwengu ambapo huwezi kabisa kuikimbia Huawei."
–Brennan Grinon (the Former U.S Defense Dept official)
–Brennan Grinon (the Former U.S Defense Dept official)
- Pentagon bado inafanya kazi na defense contractors ambao wanatumia components na huduma za kampuni ya Huawei.
- Bado wataalamu wa masuala ya kijeshi, ulinzi na usalama wa Marekani wanatumia Huawei networks kwenye shughuli zao muhimu sehemu mbalimbali duniani.
- Mpango huu unagharamiwa kifedha na serikali ya Marekani. Lakini mpaka sasa fedha zinazotolewa hazikidhi mahitaji. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, miaka minne baada ya Bunge la Congress kuamuru watoa huduma za mawasiliano na mtandao wa nchini humo kuondoa vifaa vya simu na intaneti kutoka kwa makampuni ya China, bado kuna vifaa vingi vya Huawei na ZTE ambavyo havijabadilishwa. Hawawezi kukamilisha kuondolewa kwa vifaa vya Huawei na ZTE kutokana na upungufu wa fedha wa dola bilioni 3.
- Mpaka sasa Marekani haijapata mbadala kamili atakayechukua nafasi ya Huawei kutoa huduma na vifaa kwa gharama nafuu. Hii imepelekea mataifa ambayo ni washirika wa Marekani kujiondoa kwenye mpango huu. Nchi kama UAE imekataa ombi la Marekani la kuachana na huduma za Huawei katika idara zake nyeti ambazo zina ushirika na Marekani. Nchi za Saudi Arabia na Latin America pia hazijaunga mkono.
- Pentagon inaamini kwamba ikiwa vikwazo vyote vilivyoainishwa kuhusiana na Huawei vitatimizwa, kutavuruga pia uwezo wa Pentagon wa kununua kiasi kikubwa cha vifaa vya matibabu, dawa, nguo na aina nyingine za usaidizi wa vifaa jeshi linategemea.
"Sheria hii ya bunge ilikuwa na nia nzuri sana, lakini hatukujua utekelezaji na matokeo ya kile ingemaanisha ingekuwa vigumu, mimi binafsi nadhani hilo haikufikiriwa kabisa."
–Brennan Grinon (Former Defense Dept official)
Katika miezi 3 ya mwanzo ya mwaka 2024 (Jan-Mar), kampuni ya Huawei imepata ongezeko la faida la 564% katika biashara zake. Hili limekuwa pigo kubwa sana kwa Marekani kwa sababu imeenda kinyume kabisa na matarajio yake ilipoiwekea vikwazo kampuni hiyo.
Huawei is growing stronger and less vulnerable.
Je, unafikiri Trump akichaguliwa kuwa raisi wa Marekani atakuja kufanikiwa kukimaliza kiporo alichokiacha ambacho Biden kimemshinda pia?
CREDIT: Bloomberg