Japan ni nchi tajiri kuliko China
China ina uchumi mkubwa kuliko Japan ila ukilinganisha na population yao maana yake serikali ina kazi kubwa ya kugawa resources zake kila kona ya China ili kufit population. Kwa upande mwingine Japan hizo trillion 4.4 ni nyingi kuliko population yao.
Mfano kama familia tatu (watu 15) zikiunganisha utajiri wao ukawa milioni 50, halafu kuna familia moja 1 (watu 5) yenyewe ina TSh milioni 30. Obviously hiyo familia 1 ni tajiri kuliko hizo familia tatu kwa sababu licha ya kutofikia familia 3 kwa pesa, hii familia moja ina watu wachache wa kuhudumia kuliko familia 3 zilizoungana. Familia hii moja inaweza kuhakikisha kuwa wote wanakula vizuri kuliko hizo familia 3
Ndio kama China na Japan sasa. Kuna sababu inayofanya uone China kuna restaurant, hotels au malls nyingi za bei rahisi kuliko Japan licha ya China kuwa na uchumi mkubwa zaidi. Hii maana yake ni kwamba bado kuna Wachina wengi ambao wana uwezo mdogo wa ku afford expensive life, ingawa malls za kitajiri zipo China pia, wakati Japan malls nyingi ni expensive na kupata hizo za bei ya chini ni nadra sana kwa sababu per capita income ya Japan ni kubwa.
Kutokana na population kuwa kubwa China, bado wana safari ndefu kufikia maisha ya Japan sasahivi.
Mpaka kufikia sasa kwa data za Human Development Index, kwenye nchi zinazoongoza kwa kuwa na maisha bora duniani Japan ni ya 24 wakati China ni ya 75
Ni kama ukijiuliza kwa nini Luxembourg ndio nchi tajiri zaidi duniani wakati USA ndio ina uchumi mkubwa kuliko nchi zote. Ni kwa sababu per capita income ndio inarahisisha kujua nchi ipi ni tajiri zaidi.
Canada ni nchi tajiri kuliko India. Lakini India ina uchumi mkubwa kuliko Canada. Kwa nini?
Hapo pia ndio inaturudisha kwenye fact. Japan ni nchi tajiri kuliko China. Ila China ina uchumi mkubwa kuliko Japan? Jibu ni ler capita income
Tunalinganisha pato la nchi yako na population ya nchi yako