Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Sept 11, 2024, Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani liliidhinisha kiasi cha $1.6 Billion.
- Bajeti hiyo ni ya miaka mitano (2023-2027) kueneza propaganda dhidi ya China sehemu mbalimbali duniani ikilenga hasa kuiharibia sifa China, ikitumia media za nje ya Marekani. Mpango huu umepewa jina la code H.R. 1157. Kwa wastani ni $1 million kwa siku, ili kufanikisha hilo Marekani imepanga pia kutumia ushawishi wa USAID.
Tangu mwaka 2018 kipindi Trump akiwa raisi, Marekani imekuwa katika vita kali ya kiuchumi na kuzuia ushawishi wa China. Lakini mpaka kufikia sasa ukweli ni kwamba Marekani haijaona matokeo ambayo walikuwa wanayatazamia, kwa sababu uchumi wa China haujatikisika.
Badala ya kuwekeza kwenye production na miundombinu ya Marekani inayochakaa kila uchwao, tatizo la homelessness na drugs wameamua kutumia mabilioni hayo ya pesa za walipa kodi wa Marekani kwenye propaganda dhidi ya China.
Sasa tuangazie lengo kuu hasa la mpango huu;
Kuziwezesha kifedha media, journalists, wachambuzi na propagandists katika mataifa mbalimbali watoe taarifa hasi kuhusu China.
Badala ya kuwekeza kwenye production na miundombinu ya Marekani inayochakaa kila uchwao, tatizo la homelessness na drugs wameamua kutumia mabilioni hayo ya pesa za walipa kodi wa Marekani kwenye propaganda dhidi ya China.
Sasa tuangazie lengo kuu hasa la mpango huu;
Kuziwezesha kifedha media, journalists, wachambuzi na propagandists katika mataifa mbalimbali watoe taarifa hasi kuhusu China.
- Usishangae unapoona taarifa kutoka hata mainstream-media na waandishi au wachambuzi wakiripoti habari zenye mtazamo hasi kuhusu China, ujue ni H.R. 1157 iko kazini ili kuzuia ushawishi wa China.
BRI ndiyo imelengwa hasa.
- Belt and Road Initiatives ni mkakati wa kimataifa wa maendeleo ya miundombinu uliopitishwa na serikali ya China mwaka 2013 kuwekeza katika nchi zaidi ya 150 na mashirika ya kimataifa. BRI imeifanya China iwe na ushawishi mkubwa sana duniani.
- Marekani ilijaribu kuanzisha Build Back Better World au B3W Initiatives dhidi ya BRI lakini ikabuma. Inachotaka Marekani ni kuanzisha mijadala au public opinion pressure ili kuweka shinikizo China iachane na miradi yake ya BRI na kuzishawishi nchi husika ziachane na BRI.
- Kwa mfano wanaweza kutunga negative impacts za uwekezaji wa BRI au kunzisha jumbe dhidi ya wakandarasi wa Kichina wanaojenga miundombinu katika BRI ili kuwagombanisha na wenyeji.
Lakini je, wataweza? Dunia imeshashtukia mchezo wa Marekani period.
"Makamu wa rais wa Marekani (Kamala Harris) alikuja Zambia. Alitua kwenye uwanja wa ndege uliojengwa na Wachina nchini Zambia akapita kwenye barabara iliyojengwa na Wachina nchini Zambia. Mahali pa mkutano huo ni jengo lililojengwa na serikali ya China kama zawadi kwa Zambia na ajenda kuu ya mkutano huo ilikuwa kuzuia ushirikiano wa Afrika na China."
–Akende M'memb (Director of Pan-Africanism Today)
Ukweli ni kwamba hii ndio silaha ya mwisho ya Marekani dhidi ya China na atashindwa. Unafikiri baada ya hapo atatumia silaha gani? Huenda Marekani ikafanya juu chini izame ndichi kuzichapa na China na mbuzi wa kafara ni Taiwan.