China wameweza kutengeneza jua la bandia [artificial sun]

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2022
Posts
2,396
Reaction score
2,598
- Wanasayansi wa China wemeweza kutengeneza jua la bandia kwa ajili ya kuuzalisha umeme.picha[emoji116]

- Jua la bandia [ Artificial Sun ] hiki Ni kinu cha kuzalisha umeme kinachofanya kazi kwa nguvu ya nuklia[nuclear fusion].

- Mfumo wa ufanyaji kazi wake ni katika mfumo wa nuclear fusion ambapo isotopes za hydrogen [ deuterium ] ambazo huchomwa mpaka kufikia 120million celcius joto lake mpaka inakuwa plasma alafu baadae wanaongeza pressure ndani ya kinu mpka kufikia nyuzi joto 150 million celcius linakuwa na joto kuliko jua hili kawaida.

- Joto linalopatikana kwenye Hilo jua la bandia Lina joto kubwa Mara tano la joto la jua la kawaida.

- Dhumuni la kutengenezwa kwa jua Hilo la bandia / Kinu hicho ni kuzalisha umeme katika njia iliyo safi isiyochafua mazingira mfano makaa ya mawe , mafuta n.k.

- Dhumuni lengine ni kuzalisha umeme wenye nguvu kubwa kwa muda mrefu.

- Jua hilo la bandia la china/ Artificial sun of China/Kinu cha kuzalisha umeme kwa njia ya nuclear fusion kimejengwa chini ya ardhi, sehemu inayoitwa Chengdu Southwest China's sichuan province.

- Habari soma zaidi kupitia vyombo hivi vya habari. Picha[emoji116]

Hilo jua litawekwa wapi?

Angani?

Halafu kama lingekuwa na joto zaidi ya jua la asili basi hata huku lingetufikia, yani wangeanza wananchi kutoka pande tofauti tofauti za dunia wakilalamika ongezeko la joto

Halafu baadaye ndio wangekuja na tamko rasmi kuwa msiogope hilo joto limetokana na jua ambalo tumelitengeneza
 
Hoja nzuri.
 
Soma habari ndugu ilo jua sio la kuwekwa angani ilikuleta nishati ya mwanga duniani la hasha bali ni kwa kazi za kuzalisha umeme wenye nguvu ulio safi na salama dhidi ya mazingira kwa ajili ya nchi ya china
 
Nadhani litakuwa kosa la uchapaji, kwamba deuterium inachomwa na kutengeneza joto la 150 milionCelsius kisha wanawekaga mgandamizo unaopandisha joto na kuwa 120 milionCelsius., (150-120)?????
 
Nadhani litakuwa kosa la uchapaji, kwamba deuterium inachomwa na kutengeneza joto la 150 milionCelsius kisha wanawekaga mgandamizo unaopandisha joto na kuwa 120 milionCelsius., (150-120)?????
Nikutoka 120-150[emoji106]
 
Nadhani litakuwa kosa la uchapaji, kwamba deuterium inachomwa na kutengeneza joto la 150 milionCelsius kisha wanawekaga mgandamizo unaopandisha joto na kuwa 120 milionCelsius., (150-120)?????
Typing error
 
Hebu tengua kauli kwanza, kutengeneza Jua?. Habu tujaribu kutumia elimu tuliyoipata vizuri.
 
Soma habari ndugu ilo jua sio la kuwekwa angani ilikuleta nishati ya mwanga duniani la hasha bali ni kwa kazi za kuzalisha umeme wenye nguvu ulio safi na salama dhidi ya mazingira kwa ajili ya nchi ya china
Kwa nini liitwe jua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…