Disemba 12, China ilirusha kwa mafanikio satelaiti mbili za majaribio, Shiyan-20A na Shiyan-20B, kwa kutumia roketi ya LongMarch 4C kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Jiuquan. Satelaiti hizo mbili zitatumika kufanya majaribio ya teknolojia mpya za kusimamia mazingira ya anga ya juu.